Home International KLOOP HAAMINI MACHO YAKE WAKITINGA FAINALI LIGI YA MABINGWA

KLOOP HAAMINI MACHO YAKE WAKITINGA FAINALI LIGI YA MABINGWA

JURGEN Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool amesema kuwa kuweza kufika hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ni kupata uzoefu mpya kwa kuwa wachezaji wake waliweza kufanya jambo ambalo limemshangaza.

Ilikuwa ni kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali ya pili, Liverpool walitoka nyuma mbele ya Villarreal na kushinda kwa jumla ya mabao 5-2.

Villarreal wakiwa nyumbani walianza kupachika bao dakika ya 3 kupitia kwa Boulaye Dial na bao la pili lilipachikwa na Francis Coquelin dk ya 41.

Liverpool iliweza kupindua meza kipindi cha pili kwa kuanza kupachika bao kupitia kwa Fabinho dk ya 62 kisha usawa uliwekwa dakika ya 67 na Luis Diaz na ngoma ya ushindi ilikamilishwa na Sadio Mane dk ya 74.

Villarreal walipata pigo la mchezaji wao mmoja kuonyeshwa kadi nyekundu alikuwa ni Ettienne Capoue dk ya 85.

Liverpool sasa inakwenda fainali nchini Ufaransa ambapo inatarajiwa kucheza na Real Madrid ama Manchester City ambao watacheza mchezo wao wa nusu fainali ya pili leo Jumatano.

Previous articleYANGA YAZIPIGIA HESABU POINTI ZA RUVU SHOOTING
Next articleNAHODHA YANGA ASAINI MIAKA MIWILI