Home Sports NAMNA YANGA NA SIMBA WALIYVOWAPA MKWANJA TFF

NAMNA YANGA NA SIMBA WALIYVOWAPA MKWANJA TFF

 KAMATI ya Uendeshaji na Usimamizi wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania imetoa adhabu baada ya kupitia matukio ambayo yalikuwa kwenye mechi zilizochezwa hivi karibuni.

Hii ni kwenye Ligi Kuu Bara, Championship na kuna timu ambazo zilikutwa na hatia kisha zikapigwa adhabu kutokana na makossa ambayo waliyafanya.

Ripoti inaonyesha kwamba Yanga imepigwa faini y ash.2,000,000 kwa kosa la kupita mlango usio rasmi kwenye mchezo dhidi ya Azam FC uliochezwa Azam Complex,Aprili 6.

Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo huo Yanga iliweza kupata ushindi wa mabao 2-1 na kupata alama tatu muhimu.

Pia adhabu nyingine ni ile ya mashabiki wa Yanga kuwapiga waamuzi kwa chupa wametozwa pia faini ya 1,000,00 kwa kosa hilo la kumtupia mwamuzi chupa za maji.

Hata mashabiki wa Simba nao walitupa chupa za maji kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union baada ya mashabiki kutupa chupa za maji pale Meddie Kagere alipoweza kufunga ilikuwa Aprili 7,2022.

Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Mkwakwani,Tanga na adhabu hii ni kwa mujibu wa vifungu ambavyo vipo.

Ukiachana na wakongwe Simba na Yanga hata Mbeya Kwanza nao wamekutana na adhabu ambapo wao wamepigwa faini ya 500,000 kwa kosa la mashabiki na viongozi kuingia uwanjani.

Hiyo ilikuwa baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union na Geita Gold nao wamepigwa faini ya 1,000,000 kwa kosa la mashabiki kuvamia chumba cha kubadilishia cha KMC na kumpiga mtunza vifaa.

Alikuwa ni Yahya Tostao na Ofisa Usalama,Peter Kuzungura na kuiba jezi zenye thamani y ash 750,000 na fedha taslimu sh 250,000.

Previous articleYANGA KUINGIA KAZINI KWA MARA NYINGINE TENA
Next articleKAZE:TUTAPAMBANA KUPATA POINTI TATU