Home International FULHAM YAGAWA KIFURUSHI CHA WIKI

FULHAM YAGAWA KIFURUSHI CHA WIKI

KLABU ya Fulham imetwaa ubingwa wa Ligi Daraja la Kwanza nchini Uingereza maarufu kama Championship.

Fulham imechukua Ubingwa huo ikiwa katika Uwanja wake wa nyumbani Craven Cottage kwa kuichakaza Luton kwa jumla ya mabao 7-0.

Fulham iliyoshuka daraja msimu uliopita kwa matokeo hayo sasa inapanda daraja na kurudi katika Ligi Kuu nchini Uingereza.

Imecheza jumla ya mechi 45 ikifanikiwa kukusanya jumla ya alama 90 huku ikiwa imebakiwa na mchezo mmoja mkononi kukamilisha jumla ya michezo 46.

Kwa Upande mwingine mfungaji kinara wa mabao katika mashindano hayo raia wa Serbia Alexander Mitrovic amevunja rekodi iliyowekwa na Guy Whittingham ya mabao 42.

Yeye alitupia mabao manne katika ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Luton na kufikisha jumla ya mabao 43 akiwa ndiyo kinara wa ufungaji katika msimamo wa wafungaji wa Ligi ya Daraja la kwanza nchini Uingereza.

Previous articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMANNE
Next articleKIBWANA,SAIDO BADO HAWAJAPEWA MIKATABA