
MABOSI NAMUNGO FC WAPEWA DAKIKA 90
MCHEZO wa Namungo FC dhidi ya Ruvu Shooting umeshikilia hatma ya Kocha Mkuu, Hemed Morocco na Mtendaji Mkuu, Omary Kaaya. Kwa mujibu wa Kamati Tendaji ya Namungo na mwenyekiti wake ni Hassan Zidadu imekubaliana kufanya hivyo baada ya kukaa kikao Jumatatu ya Novemba 29. Zidadu ameweka wazi kuwa wamekuwa na mwendo ambao hauridhishi katika timu…