Home Sports YANGA KAZINI TENA DHIDI YA MBEYA KWANZA

YANGA KAZINI TENA DHIDI YA MBEYA KWANZA

 VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga wanaonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi Ijumaa watakuwa kwenye msako wa pointi tatu.

Ni mchezo wa ligi dhidi ya Mbeya Kwanza utakaochezwa Uwanja wa Mkapa saa 1:00 usiku.

Awali mchezo huo ulitarajiwa kuchezwa Jumamosi ya Mei 21 sasa ngoma itapigwa Mei 20, Uwanja wa Mkapa.

Yanga imetoka kushinda mabao 2-0 dhidi ya Dodoma Jiji na Mbeya Kwanza imetoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Geita Gold, Uwanja wa Majimaji,Songea.

Enock Jiah wa Mbeya Kwanza anatarajiwa kukosekana kwenye mchezo huo baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo uliopita dhidi ya Geita Gold.

Previous articleAZAM V SIMBA KITAWAKA LEO DK 90 ZA KAZI
Next articlePABLO ACHIMBA MKWARA WA UBINGWA YANGA