JEMBE AMPA UJUMBE HUU FEI KUHUSU CHAMA
WASEMA kweli nchi hii hawapendwi, ukweli mara nyingi unaumiza lakini ukiukubali ni dawa. Mjadala wa ubora, nani zaidi kati ya Chama na wewe unazidi kukua lakini kwangu naona umejawa ushabiki zaidi ya uhalisia. Watu wanakwita Zanzibar Finest lakini kama ni kiungo mchezeshaji wewe ni Tanzania Bara na Visiwani Finest…lakini tumtoe Chama. Mashabiki wake wanamuita Mwamba…