Home Uncategorized SERIKALI KUBORESHA VIWANJA,MPOLE APEWA TUZO YAKE

SERIKALI KUBORESHA VIWANJA,MPOLE APEWA TUZO YAKE

LEO Julai 7 siku ya Sabasaba ikiwa ni usiku wa Tuzo kwa msimu wa 2021/22 Serikali imetaja viwanja ambavyo vitafanyiwa maboresho.

Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mohamed Mchengerwa ametaja viwanja sita vitakavyokarabatiwa na Serikali kwa kuwekewa nyasi za asili.

Viwanja hivyo ni pamoja na CCM Kirumba Mwanza, Sheikh Amri Abeid Arusha, Sokoine Mbeya, Mkwakwani Tanga, Jamhuri Dodoma na Amaan Zanzibar.

Mchengerwa ameweka wazi kwamba maboresho hayo ni ya kimkakati na lengo kubwa ni kuona kwamba sekta ya michezo inasonga mbele.

Aidha amewasisitiza wanafamilia ya michezo hasa timu kuweza kutimiza lengo la kuwa na uwanja kwa kila timu.

Katika usiku wa tuzo za leo tayari tuzo zimeanza kutolewa ambapo ile ya mfungaji bora amekabidhiwa staa wa Geita Gold ambaye ni George Mpole.

Mpole alitupia mabao 17 na pasi nne kwenye ligi akiwa ndani ya Geita Gold ambayo imegota katika hatua ya nne kwenye ligi.

Ni katika usiku wa tuzo za TFF unaoendelea muda huu,

Previous articleAZAM FC YAACHANA NA BEKI WAO WA KAZI
Next articleHIKI HAPA RASMI KIKOSI BORA 2021/22 LIGI KUU BARA