Home Sports AZAM FC YAACHANA NA BEKI WAO WA KAZI

AZAM FC YAACHANA NA BEKI WAO WA KAZI

LEO Julai 7,2022 ikiwa ni siku ya sabasaba,matajiri wa Dar wameweka wazi kuwa wanaachana na mchezaji wao Yvan Mbala ambaye ni beki.

Anakuwa ni nyota wa tatu kupewa mkono wa asante baada ya Mathias Kigonya ambaye na kipa pamoja na Frank Domayo ambao wote hawatakuwa kwenye kikosi cha Azam FC msimu wa 2022/23.

Kupitia ukurasa rasmi wa Insta wa Azam FC wameachia ujumbe huu:”Tumefikia makubaliano ya pande mbili ya kuachana na aliyekuwa beki wetu wa kati, Yvan Mballa.

“Mballa alijiunga nasi msimu uliopita akitokea Forest Rangers ya Zambia, kwa mkataba wa mwaka mmoja.

“Tunamshukuru kwa mchango wake, na tunamtakia kila la kheri katika maisha yake mapya ya soka,”.

Previous articleKIKOSI BORA CHA LIGI KUU BARA 2021/22
Next articleSERIKALI KUBORESHA VIWANJA,MPOLE APEWA TUZO YAKE