KIKOSI BORA CHA LIGI KUU BARA 2021/22

    ULE ubora wa wachezaji umeonekana kwa msimu wa 2021/22 kila aliyepewa nafasi alifanya kweli na mwisho wa siku kila mmoja kavuna kile ambacho amekipata.

    Wakati leo Julai 7 Bodi ya Ligi Tanzania wakitarajia kutoa tuzo kwa wachezaji waliofanya vizuri pamoja na kutangaza kikosi bora,hapa tunakuletea kikosi bora kwa msimu wa 2021/22.

    Mfumo utakaotumika ni ule wa 4-3-3 ambao unatumia mabeki wanne,viungo watatu na washambuliaji watatu,Kocha Mkuu atakuwa ni mzawa Felix Minziro na msaidizi wake atakuwa ni Malale Hamsini wa Polisi Tanzania,namna hii:-

    Diarra

    Djigui Diarra anaingia langoni kutimiza majukumu yake akiwa ni kinara kwa makipa ambao hawajafungwa mabao mengi msimu wa 2021/22.

    Ndani ya Yanga ameweza kucheza mechi 22 na kuyeyusha dk 1,944  hajafungwa kwenye mechi 15 akiwa amefungwa mabao 7 na katika mabao hayo ni bao moja amefungwa kwa penalti ilikuwa mbele ya Mbeya City, Uwanja wa Sokoine.

    Kwa mabeki itakuwa namna hii:-

    Djuma Shaban

    Atakuwa na kazi zaidi ya moja uwanjani,kulinda,kukaba,kupandisha mashambulizi pamoja na kupiga yale mapigo huru kwenye kikosi hiki.

    Djuma Shaban wa Yanga anaongoza kwa mabeki waliomwaga maji mara nyingi akiwa ametoa jumla ya pasi tano za mabao na amefunga mabao matatu kwenye ligi.

    Nyota huyo amecheza mechi 24 kasepa na dk 2,085 akiwa amekosekana kwenye mechi 6 kwa msimu huu.

    Mohamed Hussein

    Muite Tshabalala beki wa kazi ngumu ndani ya kikosi cha Simba ambaye ubora wake ni uleule akianza kikosi cha kwanza kwenye mechi za ligi na kimataifa pia huwa anakiwasha.

    Msimu huu kacheza mechi 22 za ligi katupia bao moja huku akiwa ametoa pasi mbili za msimu wa 2021/22.

    Dickson Job

    Mtu wa kazi ni Dickson Job ndani ya kikosi cha Yanga msimu huu wa 2021/22 kacheza mechi 25 katumia dk 2,241 na katoa pasi moja ya bao,licha ya umbo lake lakini anamudu kuipata mipira ile ya juu.

    Henock Inonga

    1,685 ni dakika ambazo kayeyusha beki Inonga mzee wa kukata umeme na ametupia mabao matatu ndani ya ligi msimu huu baada ya kucheza mechi 20 akiwa amekosekana kwenye mechi 10 pekee msimu huu.

    Viungo

    Yannick Bangala

    Bangala amecheza mechi 23 na kusepa na dk 2,074 ana asisti 1 anauwezo wakucheza pia katika nafasi ya ulinzi kijana huyu ambaye amekuwa kwenye mwendo bora kila anapoanza.

    Feisal Salum

    Feisal Salum wa Yanga ametupia mabao 6 na kutoa pasi nne za mabao akiwa amecheza mechi 26 na kuyeyusha dk 2,071 msimu huu wa 2021/22.

    Shiza Kichuya

    Nyota wa pili kufunga hat trick ndani ya ligi kwa msimu wa 2021/22 baada ya ile ya kwanza kufungwa na Jeremia Juma wa Tanzania Prisons.

    Kichuya alifunga mbele ya Mtibwa Sugar na nyota wa tatu kufunga hat trick alikuwa ni Idrisa Mbombo wa Azam FC.

    Kiungo huyu msimu huu kafunga mabao 8 na ametoa jumla ya pasi mbili za mabao yupo zake Namungo.

    Washambuliaji

    George Mpole

    Mzawa namba moja ambaye ni mfungaji bora kwa msimu wa 2021/22 baada ya kutupia kambani mabao 17 na pasi nne za mabao.

    Akiwa zake ndani ya kikosi cha Geita Gold ameanza kikosi cha kwanza kwenye mechi 24 ambapo mechi moja aliweza uwa super sub alifunga mbele ya Mbeya City.

    Fiston Mayele

    Mayele katupia mabao 16 na pasi tano za mabao huku na amecheza mechi 30 moja ya wachezaji ambao hawajaonyeshwa kadi ile ya njano wala nyekundu katika dk 2,373 ambazo amezitumia msimu huu.

    Rodgers Kola

    Staa wa Azam FC mwenye zali la kuwatungua Yanga na Simba bao mojamoja,huyu ni miongoni mwa washamuliaji ambao wanapenda kufunga.

    Katupia mabao 9 ameanza kikosi cha kwanza mechi 14 na ametoa pasi mbili za mabao.

    Imeandikwa na Dizo Click

    Previous articleMWAMBA WA LUSAKA AANZA KUPIGA MATIZI
    Next articleAZAM FC YAACHANA NA BEKI WAO WA KAZI