Home Sports MWAMBA WA LUSAKA AANZA KUPIGA MATIZI

MWAMBA WA LUSAKA AANZA KUPIGA MATIZI

MWAMBA wa Lusaka kiungo mshamuliaji wa Simba,Clatous Chama ameanza kufanya mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa 2022/23.

Chama amerejea kwa mara nyingine ndani ya Simba baada ya kuwa ndani ya RS Berkane lakini ameshindwa kuonyesha makeke yake kutokana na kile kilichoelezwa kuwa alipata maumivu kwenye mchezo dhidi ya Yanga.

Taarifa iliyotolewa na Simba imeweka wazi kuwa tayari kiungo huyo ambaye alitoa pasi 15 za mabao msimu uliopita ameanza mazoezi kwa ajili ya msimu mpya ujao.

Simba msimu huu imekwama kuvunja rekodi zake ambazo iliziweka msimu uliopita baada ya kuwa na mwendo wa kinyonga kwenye kila idara.

Ikumbukwe kwamba kwa msimu wa 2020/21 tuzo ya kiungo bora ilikuwa mikononi mwa Chama lakini kwa msimu huu wa 2021/22 inatarajiwa kwenda kwa nyota kutoka Yanga.

Previous articleKIUNGO NUNES APIGIWA HESABU CHELSEA
Next articleKIKOSI BORA CHA LIGI KUU BARA 2021/22