JEMBE AMPA UJUMBE HUU FEI KUHUSU CHAMA

    WASEMA kweli nchi hii hawapendwi, ukweli mara nyingi unaumiza lakini ukiukubali ni dawa.

    Mjadala wa ubora, nani zaidi kati ya Chama na wewe unazidi kukua lakini kwangu naona umejawa ushabiki zaidi ya uhalisia.

    Watu wanakwita Zanzibar Finest lakini kama ni kiungo mchezeshaji wewe ni Tanzania Bara na Visiwani Finest…lakini tumtoe Chama.

    Mashabiki wake wanamuita Mwamba wa Lusaka, si Mtanzania kama mimi na wewe lakini ni fundi wa mpira, hata fundi kama wewe unakubaliana nami.

    Angalia mashabiki wasikuondoe njiani kwa kukupa daraja unalopambana kulifikia…Kuna mengi bado na kuna rekodi zake nyingi huna….Chama ado OVERSIZE kwako.

    Ubora wako unapanda na nikusifu kwa kutunza kiwango na leo tunakusifia kwa mchango mkubwa wa kuifikisha Yanga hatua ya makundi Kombe la Shirikisho, Chama kaisaidia Simba kufika hatua hiyo Ligi ya Mabingwa Afrika mara tatu (hapa labda miaka mitano ijayo).

    Tunakusifia kuisaidia Yanga kuwa bingwa Bara na Shirikisho, yeye kaisaidia Simba kuwa bingwa mara nne (Bara), mbili (Shirikisho)-Labda miaka mitatu ijayo.

    Uwezo wa Chama unaujua, umeshakutana naye, bado unakua kimpira, huku UTAFIKIA TU. usikubali WAKUHARAKISHE…safari ni hatua…

    NIKUKUMBUSHE, hata WANAOKUHARAKISHA wanaujua ubora wa Chama…walishaunadi ubora huo, walielezea na walieleza…Mimi naamini siku itafikia UTAFIKIA na ikiwezekana UTAVUKA lakini sio leo WALA MSIMU UJAO…..Keep going..

    Previous articleVIDEO:MZARAMO ATEMA CHECHE,ATAJA MABAO YA MAYELE YA MCHONGO
    Next articleMEDDIE KAGERE AKUBALI MUZIKI WA YANGA