
MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATATU
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Championi Jumatatu
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Championi Jumatatu
WAWAKILISHI wa Tanzania, Simba kwenye hatua ya Kombe la Shirikisho safari yao imefika mwisho leo nchini Afrika Kusini baada ya kufungwa kwa mikwaju ya penalti. Ngoma ilikuwa nzito hasa kipindi cha kwanza, Simba walipiga mpira mkubwa kwa kujilinda huku viungo wakishindwa kutengeneza nafasi kwa mshambuliaji Chris Mugalu. Kadi ya njano ya Mugalu ile ya pili…
ORLANDO Pirates wakiwa nyumbani wamewatungua Simba bao 1-0 kwenye mchezo wa robo fainali Kombe la Shirikisho. Kipindi cha pili Simba walifungwa bao hilo na kuwafanya wakwame kupata ushindi. Ni baada ya Chris Mugalu kuonyeshwa kadi nyekundu. Sasa mshindi anatafutwa kwa mikwaju ya penalti.
MCHEZO wa Kombe la Shirikisho kwa sasa hatua ya robo fainali ambapo wawakilishi wa Tanzania Simba wapo kazini ni mapumziko. Dakika 45 za mwanzo zimekamilika huku ubao ukisoma Orlando Pirates 0-0 Simba. Licha ya Simba kutokufungwa bado wapo kwenye ugumu mkubwa wa kushambuliwa kwa kasi na wapinzani wao. Chris Mugalu yupo kwenye ulinzi mkubwa na…
KIKOSI cha Simba Queens leo kimechapwa bao 1-0 dhidi ya watani wao wa jadi Yanga Princess kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Soka ya Wanawake. Ilikuwa ni mchezo mkali ndani ya Uwanja wa Mkapa ambapo timu zote zilianza kwa kushambulia. Ilikuwa dk ya 5 Simba Queens walipata pigo baada ya beki wao tegemeo Singano Julieth…
BINGWA wa Dunia mara 7 katika mashindano ya uendeshaji wa magari ya Langalanga maarufu kama Formula 1 Sir Lewis Hamilton pamoja na Bingwa namba moja katika mchezo wa tenesi kwa wanawake Serena Williams kwa pamoja wameweka kitita cha Paundi milioni 20 ili kuwa wamiliki wapya wa Klabu ya Chelsea. Wanamichezo hao maarufu wameingia ubia kwa…
PABLO Franco,Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa leo watajaribu kushinda mbele ya Orlando Pirates kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho. Saa 1:00 usiku, wawakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa ambao ni Simba wana kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Orlando Pirates. Huu ni mchezo wa hatua ya robo fainali ukiwa ni wa pili baada…
LIGI ya Beach Soccer inayodhaminiwa na Global Radio na Global TV Online jana April 23 imeendelea katika Viwanja vya Coco Beach kulikuwa na michezo mitatu ya kundi A na leo tena inatarajiwa kuendelea. Mchezo wa kwanza ulikamilika na Savanah Boys iliibuka na ushindi wa mabao 6-4 Ilala FC. Mchezo wa pili Kundi A ulikuwa na…
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Spoti Xtra Jumapili
BAADA ya dakika 90 kukamilika Uwanja wa Mkapa, kikosi cha Yanga kimeituliza Namungo FC kwa kuichapa mabao 2-1. Ulikuwa ni mchezo mzuri wenye kasi ya ajabu mwanzo mwisho huku mikono ya makipa ikiwa kwenye harakati za kuokoa hatari zile za washambuliaji. Fiston Mayele alifungua akaunti ya mabao Uwanja wa Mkapa ilikuwa dk ya 17 kisha…
KOCHA wa muda ndani ya kikosi cha Manchester United Ralf Rangnick amesema kuwa kwa sasa hawezi kuzungumza kuhusu hatma ya kiungo wa timu hiyo Paul Pogba. Wakati huo pia Rangnick anaamini kwamba Erik ten Hag ambaye amepewa kandarasi ya kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo ni moja ya makocha wazuri ambao United imewapata. “Nina uhakika…
SALUM Abubakar Salum, ‘Sure Boy’ kiungo wa kazi ndani ya kikosi cha Yanga ameweka wazi kwamba anaufikiria mchezo wao dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa Aprili 30. Sure Boy aliweza kuwaka mbele ya waajiri zake wa zamani Azam FC kwenye mchezo wa ligi walipokutana Aprili 6,2022 wakati ubao wa Azam Complex uliposoma Azam…
KUMEKUCHA sasa leo ni Yanga v Namungo, Uwanja wa Mkapa ngoma inatarajiwa kupigwa ikiwa ni Aprili 23,2022. Kazi kubwa ni kwa vinara Yanga wenye pointi 51 watakapokuwa wakimenyana na Namungo FC iliyo na pointi 29 ndani ya ligi. Ugumu wao huwa unakuwa namna hii:- Wakali wa nyavu Kwa Yanga wao wanaye mzee wa kutetema, Fiston…
NYOTA wa Namungo, Relliats Lusajo leo anafikisha siku ya 62 bila kufunga bao ndani ya mechi za Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2021/22. Nyota huyo mzawa alianza kwa kasi matata na aliweza kuwa namba moja kwa muda kwa watupiaji wa ligi alipofikisha mabao 10 kibindoni. Mara ya mwisho Lusajo kufunga ilikuwa ni Februari 21,2022…
IKIWA leo wanatarajiwa kukutana Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Yanga v Namungo, Kocha Msaidizi wa Namungo, Jamhuri Kihwelo,’Julio’ amesema watapambana kufanya vizuri. Julio amebaainisha kwamba haoni sababu ya kuhofia mchezaji mmoja ama timu kiujumla kwa kuwa wamejipanga kufunga na kupata pointi tatu. Amemtaja Mayele kwamba hawezi kuwafunga leo kutokana…
KOCHA Mkuu wa Simba, Mhispania, Pablo Franco Martin anaamini mchezo wa marudiano dhidi ya Orlando Pirates utakuwa mgumu lakini ataingia uwanjani kwa mbinu tofauti ya kupata bao la mapema ndani ya dakika 10 hadi 15 za mwanzoni. Timu hizo zinatarajiwa kuvaana kesho Jumapili katika mchezo wa marudiano wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika…
Burudani ya soka inanoga zaidi wakati huu ambao msimu unaelekea ukingoni. Timu zinapambana kumaliza msimu kwenye nafasi za juu, nani atatusua na nani atavurunda? Mchongo wa wiki upo hivi; Ile burudani ya kuisaka Top 4 kwenye EPL ndio inapamba moto Jumamosi hii. Arsenal kuwaalika Manchester United ndani ya Emirates Stadium. Ni muendelezo wa big match…