
MORRISON ATIBUA DILI LA MCONGO,NDANI YA CHAMPIONI IJUMAA
MORRISON atibua dili la Mcongo Yanga,Minziro ahofia Mpole kutua Simba ndani ya Championi Ijumaa
MORRISON atibua dili la Mcongo Yanga,Minziro ahofia Mpole kutua Simba ndani ya Championi Ijumaa
GLOBAL TV imefanya mahojiano maalum na mchezaji, Benard Morrison, kuhusiana na masuala mbalimbali yanayomuhusu ikiwemo sababu za kuondoka Simba na klabu anayoelekea. “Walinipa mapumziko maana nilikataa kusaini mkataba mpya, kama ningecheza Simba miaka 5 au 10 alafu mwisho wa siku nikarudi Ghana sina hela au kumpgia mwenyekiti naomba hela kuisaidia familia yangu sio kitu kizuri”…
Uongozi wa Yanga kupitia kwa Kaimu Mtendaji Mkuu (C.E.O) wa Senzo Mbatha amekanusha taarifa inayo sambaa kuwa Mshambuliaji wa klabu hiyo, Fiston Mayele amesajiliwa na klabu ya Kaizer Chiefs kwa mkataba wa miaka mitatu na atatangazwa hivi karibuni. Amesema Kaizer Chief na Berkane zimeonyesha kumtaka nyota huyo wa kupachika mabao Yanga. “Lakini kama klabu hatumuuzi,”…
MWANDISHI Mkongwe Afrika, Nuhu Adams leo Julai 30, 2022 kupitia ukurasa wake wa twitter ameandika kuwa mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele ameuzwa kwa Klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini kwa mkataba wa miaka mitatu. “South African giants Kaizer Chiefs have completed the signing of Yanga striker Fiston Kalala Mayele (28) on a three-year contract,…
PAZIA la Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wa 2021/22 jana lilifungwa rasmi baada ya viwanja vitano kutimua vumbi kwa kila timu kusaka pointi tatu muhimu. Yanga ambao ni mabingwa wa ligi waliweza kuweka rekodi yao kwa kukamilisha msimu bila kufungwa kwenye mechi 30 ambazo wamecheza. Ushindi wa bao 1-0 waliopata mbele ya Mtibwa Sugar…
MCHEZAJI wa Simba, Benard Morrison, usiku wa kuamkia Juni 29, amewasili jijini Dar akitokea nchini Ghana..
KOCHA mpya Simba aanza na Yanga,ashusha majembe ya maana apewa masharti matatu ndani ya Spoti Xtra Jumanne
KIUNGO Novatus Dismas ambaye ni winga wa timu ya Taifa ya Tanzania,Taifa Stars ameweza kupata dili la kujiunga na Klabu ya Zulte Waregen. Kiungo huyo aliwahi kucheza ndani ya kikosi cha Azam FC na alicheza pia katika Klabu ya Biashara United ambayo imeshuka daraja msimu wa 2021/22 baada ya kupoteza kwa kufungwa mabao 4-1 mbele…
MSIMU wa 2021/22 umekamilika ambapo mbivu na mbichi zimejulikana. Biashara United ya Mara itacheza Champioship msimu ujao ikiungana na Mbeya Kwanza ya Mbeya. Mtibwa Sugar wao watacheza mtoano na Tanzania Prisons ili kusaka timu itakayobaki ndani ya ligi. Matokeo yapo namna hii:- Kagera 0-0 Polisi Tanzania. Mbeya Kwanza 0-0 Simba, Yanga 1-0 Mtibwa mtupiaji ni Dennis Nkane…
LIGI Kuu Tanzania Bara leo inagota ukingoni ambapo mechi zinachezwa kwa mara ya mwisho msimu wa 2021/22. Matokeo kwa sasa ikiwa mapumziko yapo namna hii: Yanga 0-0 Mtibwa Sugar Mbeya City 0-1 Namungo Ruvu Shooting 1-0 Prisons Coastal Union 1-1 Geita Gold Azam FC 1-0 Biashara United Kagera 0-0 Polisi Tanzania Mbeya Kwanza 0-0 Simba…
NYAKATI za mashaka kwa sasa kwa baadhi ya timu na mashabiki ni sasa hasa kutokana na kushindwa kupata matokeo kwenye mechi ambazo walicheza mzunguko wa kwanza. Ukurasa wa mwisho kwa mechi ambazo zitachezwa utaamua nani atakuwa nani baada ya mwisho wa msimu kutokana na kila timu kuhitaji pointi tatu. Mbeya Kwanza asanteni kwa kuja nadhani…
KIKOSI cha Simba chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Seleman Matola leo kitakuwa na kibarua cha kusaka ushindi dhidi ya Mbeya Kwanza. Hiki hapa kikosi kitakachoanza:- Beno Kakolanya Jummsone Gadiel Onyango Kenned Lwanga Kassim Nyoni Kibu Banda Mhilu Akiba Aly Inonga Bocco Hassan Shaffi
LEO Juni 29 mabingwa wa Ligi Kuu Bara Yanga wanakamilisha mzunguko wa 30 kwa kucheza na Mtibwa Sugar. Hiki hapa kikosi cha Yanga:- Mshery Kibwana Bryson Mwamnyeto Bacca Feisal Farid Jesus Ambundo Kaseke Mayele Akiba Johora Boxer Yassin Shaibu Balama Ushindi Nkane Makambo Yusuph
KUELEKEA mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao, uongozi wa mabingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, Yanga umechimba mkwara mzito kwa kusema tayari umeanza kufanya maandalizi mazito ya ndani na nje ya uwanja kuhakikisha wanaandika rekodi ya kufika mbali katika michuano hiyo. Yanga tayari imekata tiketi ya uwakilishi wa Tanzania katika michuano ya…
ARSENAL imeboresha ofa yake kwa beki wa Ajax, Lisandro Martinez huku pia wakiwa wanatumaini kufikia makubaliano na Leeds United kuhusu Raphinha. Arsenal imeboresha ofa yake na kufikia pauni milioni 34 kwa ajili ya Muargentina Martinez lakini Ajax wanataka kiasi kinachokaribia pauni milioni 43 huku pia Man United wakiwa wanamtaka. Hata hivyo, United inahitaji kuuza kwanza…
WAMILIKI wapya wa Chelsea wakiongozwa na bilionea Todd Boehly, wameifumua bodi ya timu hiyo wakifukuza kazi vichwa kibao akiwemo gwiji Petr Cech, na hali hiyo imewafanya mashabiki kuwa na wasiwasi na kuonyesha hisia zao kwenye mitandao ya kijamii. Cech ambaye ni kipa wa zamani wa Chelsea alikuwa mshauri wa ufundi na viwango klabuni hapo tangu…
UHAMISHO wa Gabriel Jesus kutokea Man City kwenda Arsenal ulitarajiwa kutangazwa muda wowote kuanzia jana jioni baada ya jana asubuhi kutua jijini London kwa ajili ya kufanya vipimo vya afya. Mara baada ya kutua katika viwanja vya mazoezi vya Arsenal, Jesus alipokelewa na Mbrazili mwenzake, Edu ambaye alikumbatiana naye kabla ya kukamilisha uhamisho huo wa…