Home Sports HIVI NDIVYO LIGI ILIVYOKAMILIKA 2021/22,REKODI ZAO PIA

HIVI NDIVYO LIGI ILIVYOKAMILIKA 2021/22,REKODI ZAO PIA

PAZIA la Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wa 2021/22 jana lilifungwa rasmi baada ya viwanja vitano kutimua vumbi kwa kila timu kusaka pointi tatu muhimu.

 Yanga ambao ni mabingwa wa ligi waliweza kuweka rekodi yao kwa kukamilisha msimu bila kufungwa kwenye mechi 30 ambazo wamecheza.

 Ushindi wa bao 1-0 waliopata mbele ya Mtibwa Sugar umewafanya waweze kufikisha jumla ya pointi 74 wakiwa nafasi ya kwanza na mkwanja ambao watavuna bonas ya milioni 600 wakati Mtibwa wao waliomaliza ligi wakiwa nafasi ya 13 watavuna bonasi ya milioni 25.

Uwanja wa Majimaji ubao ulisoma Mbeya Kwanza 0-0 Simba na kuwafanya Mbeya Kwanza kukamilisha ligi wakiwa na pointi 25 nafasi ya 16 na watavuna bonasi ya milioni 10 huku Simba nafasi ya pili wao ni bonasi ya milioni 300 watavuta.

Play offs

 Tanzania Prisons na Mtibwa Sugar hizi zitacheza mchezo wa mtoano ili kuweza kusaka nafasi ya kubaki ndani ya ligi na mshindi wa jumla mchezo wa nyumbani na ugenini atabaki kwenye ligi na yule ambaye atapoteza atacheza na JKT Tanzania ya Championship ili kupata mshindi atakayecheza ligi.

Matokeo mengine

Coastal Union 1-1 Geita Gold,Dodoma Jiji 1-0 KMC,Ruvu Shooting 1-0 Prisons,Mbeya City 1-1 Namungo,Azam FC 4-1 Biashara United.

Hat trick ni 3

 Ligi imekamilika ikiwa na hat trick tatu ambapo ya kwanza ni ile ya Jeremia Juma wa Tanzania Prisons alifunga mbele ya Namungo, Uwanja wa Nelson Mandela,Shiza Kichuuya wa Namungo alifunga mbele ya Mtibwa Sugar na Idrissa Mbombo yeye alifunga mbele ya Biashara United.

 Biashara United yaungana na Mbeya Kwanza

 Biashara United ya Mara inakuwa timu ya pili kushuka ikiungana na Mbeya Kwanza ya Mbeya ambayo hii ilikata tiketi yake ya kushiriki Championship kabla ya mchezo wa mwisho.

Mfungaji bora

Mzawa George Mpole wa Geita Gold yeye jana alifikisha mabao 17 na kuweza kumpoteza Fison Mayele wa Yanga ambaye aligota kwenye namba 16 ya mabao.

 Wakali wa Clean Sheet

 Kipa namba moja wa Yanga Diarra Djigui yeye ni namba moja kwa kucheza mechi nyingi bila kuruhusu mabao ambazo ni mechi 15 akifuatiwa na Aboutwalib Mshery ambaye amecheza mechi 12 bila kufungwa.

 Kipa namba moja wa Simba,Aishi Manula yeye amefikisha mechi 11 bila kufungwa msimu huu wa 2021/22 ambapo timu yake imegota kwenye nafasi ya pili.

Imeandikwa na Dizo Click

Previous articleVIDEO:NAMNA MORRISON ALIVYOTUA BONGO KUONANA NA VIONGOZI SIMBA
Next articleMAYELE ADAIWA KUUZWA KAIZER CHIEFS YA AFRIKA KUSINI KWA MKATABA WA MIAKA MITATU