Home Sports MORRISON ASIMULIA SAKATA ZIMA KUONDOLEWA SIMBA, UGOMVI NA CEO, TRY AGAIN -VIDEO

MORRISON ASIMULIA SAKATA ZIMA KUONDOLEWA SIMBA, UGOMVI NA CEO, TRY AGAIN -VIDEO

GLOBAL TV imefanya mahojiano maalum na mchezaji, Benard Morrison, kuhusiana na masuala mbalimbali yanayomuhusu ikiwemo sababu za kuondoka Simba na klabu anayoelekea.

“Walinipa mapumziko maana nilikataa kusaini mkataba mpya, kama ningecheza Simba miaka 5 au 10 alafu mwisho wa siku nikarudi Ghana sina hela au kumpgia mwenyekiti naomba hela kuisaidia familia yangu sio kitu kizuri”

“Niliomba mkataba mzuri, maboresho kwenye mkataba ili niwe vizuri kuihudumia klabu na haikufanyika hivyo, nilikuwa na kikao na Barbara na sababu Ya hicho kikao ni kwa sababu tulicheza mechi dhidi ya Yanga na ile mechi nilipata majeraha na awali tayari nilikuwa majeruhi kwenye mechi dhidi ya Orlando Pirates”

“Baada ya mechi daktari hakunifuata kunihudumia wala kujua hali yangu, nilimtumia meseji nyingi kuwa sipo sawa lakini hakufanya hivyo, niliwaambia hamnijali hivyo nililazimika kujihudumia mwenyewe nikiwa nyumbani”

“CEO alinipigia simu nikaenda ofisini kwake akaniambia wachezaji wanahasira, wanasema hawataki niende tena kambini wala mazoezini, kocha analalamika siwaheshimu, hawataki niende mazoezini hivyo malalamiko ni mengi ni kwa nini nafanya hivyo ?”

“Nilimjibu sio kweli sidhani kama wachezaji wanaweza kufanya hivyo maana ndio hao hao wachezaji wananipigia simu nisipoonekana kambini kunijulia hali lakini wewe CEO unasema hivi, Bocco,

“Kocha alinipigia simu tukaongea kama dakika 40 nikamuuliza baada ya mkutano wangu na CEO unadhani kuna nini kitatokea akanijibu hadhani kama kuna namna ya mimi kurudi klabuni na kwa vile CEO aliniambia nenda ukakae nyumbani usubiri nitakupigia nikajua kuna jambo linaendelea”

“Asubuhi yake nilimpgia CEO akaniambia niende ofisini kwake, nilipoenda akaniambia mambo mawili, (i) nikubali kwenda nyumbani nikae nje ya Klabu hadi mwisho wa msimu alafu watawaambia mashabiki nimeenda nyumbani kwa matatizo ya kifamilia na nitarudi mambo yakiwa sawa au (ii) ataweka kwenye social media kuwa wamenisimamisha hadi mwisho wa msimu,” Mchezaji wa Simba, Bernard Morrison

Mkude, Chama, Bwalya walikuwa wananijulia hali kila siku,” Mchezaji wa Simba Sc, Bernard Morrison.

Previous articleSENZO AKANUSHA TAARIFA YA MAYELE KUSAJILIWA NA KAIZER CHIEFS
Next articleMORRISON ATIBUA DILI LA MCONGO,NDANI YA CHAMPIONI IJUMAA