AZAM FC BADO HAIJAFIKA KWENYE UBORA WENYEWE
KOCHA Mkuu wa Klabu ya Azam FC, Abdi Hamid Moalin, amesema bado hajaipata Azam anayoitaka na ubora wa kikosi chake kwa sasa hauzidi asilimia 65 hivyo bado jambo lao ni kusaka uimara kwa asilimia kubwa. Moalin amefunguka kuwa kuna levo ya ubora ambayo anahitaji kuiona kwenye timu yake, jambo ambalo bado analifanyia kazi kwa sasa…