
MUZIKI WA SIMBA MPYA USIPIME,KAMBOLE AOMBA JEZI NAMBA 7
NDANI ya gazeti la Championi Jumatatu habari kubwa inaeleza kuhusu muziki wa Simba mpya huku Kambole yeye akiomba jezi namba 7 Yanga
NDANI ya gazeti la Championi Jumatatu habari kubwa inaeleza kuhusu muziki wa Simba mpya huku Kambole yeye akiomba jezi namba 7 Yanga
BADO dirisha la usajili halijafunguliwa rasmi kwa sasa ila muhimu kuongeza nguvu kwenye vikosi ikiwa ni maandalizi ya msimu ujao ambao upo njiani kuweza kuanza tena. Kikubwa kwa sasa ni kuanza kupitia yale mapendekezo ya mwalimu ambayo alitoa kuna yale majalada ya wakati ule wa usajili wa dirisha dogo mahali ambapo hapakukamilishwa basi pafanyiwe kazi….
UONGOZI wa Simba umesema kuwa hauna hofu hata kama wakimkosa kiungo mshambuliaji wa ASEC Mimosas, Stephane Aziz Ki kwani wapo wachezaji bora na wazuri wengine katika timu hiyo. Simba wamejipongeza kwa kuwaleta wachezaji wazuri Bongo ikiwa ni pamoja na Aziz KI kwenye mechi za Kombe la Shirikisho, Uwanja wa Mkapa. Hiyo ikiwa ni siku chache…
IMEELEZWA kuwa nyota wa zamani wa kikosi cha Yanga, Simon Msuva yupo kwenye hesabu za mabosi wa Yanga ambao wanahitaji kumuongeza ndani ya kikosi hicho. Msuva ni winga wa kimataifa ambaye yupo Tanzania kwa sasa baada ya kuweza kutokwenda sawa na mabosi wake Wydad Casablanca ya Morocco na suala lao lipo Fifa. Nyota huyo amekuwa…
IMEELEZWA kuwa jina la Josef Vukusic ambaye amewahi kuinoa Klabu ya Polokwane na Amazulu za Afrika Kusini ambaye aliletwa duniani Agosti 3,1964 akiwa na miaka 57 anatajwa kuwa miongoni mwa makocha watakaorithi mikoba ya Pablo Franco ndani ya Simba. Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Simba zimeeleza kuwa kwa sasa mchakato huo umefika hatua nzuri…
FISTON Mayele mshambuliaji namba moja wa Yanga amesema kuwa kwa sasa hafikirii suala la tuzo ya kiatu cha ufungaji bora zaidi ya kuweza kutimiza majukumu yake. Mayele katupia mabao 16 kwenye ligi aaongoza ndani ya kikosi cha Yanga akiwa ni mchezaji mgeni mwenye mabao mengi msimu huu. Idadi hiyo ya mabao imefikiwa pia na mzawa…
KWENYE mchezo wa Ligi Kuu Bara leo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, kikosi cha Simba kimeweza kupindua meza mbele ya KMC. Pia mchezo wa leo ambao ni wa mzunguko wa pili umetumika kwa ajili ya kumuaga mchezaji wao Rally Bwalya ambaye amecheza mechi 19 na kutoa pasi tatu za mabao kuweza kuagwa kwa kuwa amepata timu…
IMEFICHUKA kuwa, mabingwa wa Ligi Kuu Bara 2021/22, Yanga SC, imewashusha kimyakimya jijini Dar es Salaam mastaa wao wawili wapya ambao ni mlinzi wa kimataifa wa DR Congo, Joyce Lomalisa na mshambuliaji wa kimataifa wa Angola, Adriano Belmiro Duarte Nicolau ‘Yano’ kwa ajili ya kukamilisha usajili wao. Taarifa kutoka chanzo chetu cha kuaminika ndani ya…
MSHAMBULIAJI wa Klabu ya Real Madrid Rodrygo Silva de Goes maarufu kama Rodrygo amebainisha kuwa wachezaji wa Real Madrid walipanga kumdhihaki mshambuliaji wa Liverpool na Timu ya Taifa ya Misri Mohamed Salah mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya maarufu kama Uefa. Mshambuliaji huyo amenukuliwa akisema:“Pale inapotokea mtu…
INAELEZWA kuwa aliyekuwa kocha wa Kaizer Chiefs na kutimuliwa kabla ya mkataba wake kuisha Stuart Baxter raia wa Uingereza (68), April 24, 2022 alifanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez. Baxter alikutana na Barbara jijini Johannesburg Simba ilipoenda kucheza na Orlando Pirates mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika na kocha huyo amesema kikao…
SI unauona moto walionao mabingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu Yanga SC? Sasa unaambiwa uongozi wa timu hiyo umetamba kuwa kwa usajili ambao wanaendelea kuufanya, basi watu wanapaswa kufahamu wanachokiona kwa sasa ni robo tu ya ubora ambao kikosi chao kitakuwa nao msimu ujao. Kuelekea msimu ujao wa 2022/23, Yanga wameanza kufanya maboresho ya…
INAELEZWA mabosi wa Simba wamepania kufanya makubwa msimu ujao kufuatia kumnasa beki wa zamani wa Chipa United, Mrundi, Frédéric Nsabiyumva. Beki huyo wa kati mwenye miaka 27, amekuwa akisifika nchini Burundi kama mmoja kati ya mabeki wa kati makatili kutokana na uwezo mkubwa alionao wa kukaba washambuliaji wasumbufu. Usajili wa beki huyo unatajwa ni sehemu…
KAMA ulikuwa huamini, basi taarifa ikufikie kwamba, Yanga imekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji wa ASEC Mimosas ya Ivory Coast, Stephane Aziz Ki na siku ya kutua nchini imetajwa. Ipo hivi, mchezaji huyo kwa taarifa za uhakika ambazo imezipata Spoti Xtra, ataingia nchini mapema ndani ya wiki ambayo inaanza kesho Jumatatu kwa ajili ya kumalizana kila…
INATAJWA kuwa beki wa kati wa Simba, Ibrahim Ame anayecheza kwa mkopo Mtibwa amegoma kuongeza mkataba kwa mabosi wake hao huku ikielezwa kuwa kuna mpango wa kujiunga na Coastal Union. Ame alijiunga na Simba msimu wa 2020/21 akitokea Coastal Union na kusaini mkataba wa miaka miwili ambao unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu. Mmoja wa…
MBWANA Samatta nahodha wa Team Samatta ameweka wazi kuwa Team Kiba wamebebwa,ilikuwa ni kwenye mchezo wa NIFUATE uliochezwa Uwanja wa Mkapa na Team Kiba wakashinda kwa penalti
DAKIKA 90 zilikuwa nzito kwa Kagera Sugar dhidi ya Dodoma Jiji kwenye mchezo wa ligi baada ya kugawana pointi mojamoja. Ilikuwa ni Uwanja wa Kaitaba ambapo mchezo huo wa ligi ulichezwa Juni 18, 2022 kwenye msako wa pointi tatu kila timu iliambulia moja. Ni bao la Wazir Junior lilikuwa la kwanza kupachikwa kimiani dk ya…