USAJILI UZINGATIE MAPENDEKEZO YA BENCHI LA UFUNDI

    BADO dirisha la usajili halijafunguliwa rasmi kwa sasa ila muhimu kuongeza nguvu kwenye vikosi ikiwa ni maandalizi ya msimu ujao ambao upo njiani kuweza kuanza tena. 

    Kikubwa kwa sasa ni kuanza kupitia yale mapendekezo ya mwalimu ambayo alitoa kuna yale majalada ya wakati ule wa usajili wa dirisha dogo mahali ambapo hapakukamilishwa basi pafanyiwe kazi.

    Pia kwa mwendo ambavyo umekwenda nina amini kwamba kila baada ya mechi huwa kunakuwa na vikao vya kamati ya ufundi wanajua tatizo lipo wapi.

    Zipo timu ambazo zimeanza kusajili wachezaji wapya na zipo ambazo zimeanza kuwaongezea mikataba wachezaji wao basi iwe ni kwa mapendekezo ya benchi la ufundi.

    Yale masuala ya nina mchezaji wangu anajua sijui huyu atatusaidia muda wake umekwisha ni zamu ya benchi la ufundi kufanya kazi.

     Kwenye karata ya msako wa bingwa wa ligi hiyo imeshafungwa kwani bingwa anajulikana ambaye ni Yanga katika hilo anastahili pongezi huku wale ambao walikuwa wakihitaji kufanya hivyo wao wakipaswa kujipanga kwa wakati ujao.

    Kilichobaki kwa sasa ni msako wa yule ambaye atashuka ambapo timu mbili zitashuka jumlajumla na mbili zitacheza mchezo wa mtoano hapo muhimu kuwekeza nguvu pale ambapo utakuwa.

     Ikiwa utaangukia kwenye sakata la kucheza mtoano basi jipange kufanya vizuri ukipoteza basi tutakutana ndani ya Championship msimu ujao.

     Kama utadondoka kwenye kushuka basi maisha yako msimu ujao yatakuwa kwenye Championship, hapo muhimu hesabu na kutimiza kile ambacho kitakuwa kwenye mpango kazi kwa msimu huo.

    Imeandikwa na Dizo Click.

    Previous articleSIMBA WAJIVUNIA KUMLETA AZIZ KI BONGO
    Next articleMUZIKI WA SIMBA MPYA USIPIME,KAMBOLE AOMBA JEZI NAMBA 7