Home Sports SIMBA WAJIVUNIA KUMLETA AZIZ KI BONGO

SIMBA WAJIVUNIA KUMLETA AZIZ KI BONGO

UONGOZI wa Simba umesema kuwa hauna hofu hata kama wakimkosa kiungo mshambuliaji wa ASEC Mimosas, Stephane Aziz Ki kwani wapo wachezaji bora na wazuri wengine katika timu hiyo.

Simba wamejipongeza kwa kuwaleta wachezaji wazuri Bongo ikiwa ni pamoja na Aziz KI kwenye mechi za Kombe la Shirikisho, Uwanja wa Mkapa.

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu picha zisambae zikimuonyesha Aziz Ki, meneja wake wakiwa na Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Injinia Hersi Said nchini Burkina Fasso.

Taarifa zilizokuwepo kuwa Yanga imemalizana na Aziz Ki kwa kusaini mkataba wa miaka miwili ya kukipiga katika timu hiyo, kwa dau la Sh mil 650.

Kwa mujibu wa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Mulamu Nghambi, amesema wapo wachezaji wengi wenye kiwango bora Afrika zaidi ya Aziz Ki na mshambuliaji wa US Gendamerie ya nchini Niger, Victorien Adebayor ambaye muda wowote atatambulishwa RS Berkane ya Morocco.

Nghambi alisema kuwa Aziz Ki na Adebayor wameonekana bora baada ya kuwafunga Simba katika michezo ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu na kuvutika na baadhi ya klabu zilizopeleka ofa.

Aliongeza kuwa ndani ya kikosi cha ASEC, yupo mshambuliaji anayeitwa Konaté mwenye kiwango kizuri zaidi ya hao akina Aziz Ki na Adebayor.

“Kwanza kabisa tujipongeze sisi Simba ambao tumewaleta wachezaji hapa nchini kutokana na kushiriki michuano ya kimataifa na kuwa kivutio kwa klabu nyingine.

“Kati ya wachezaji hao yupo Aziz Ki ambaye anatajwa sana katika usajili wa msimu ujao na taarifa zilizokuwepo anawaniwa na moja ya timu kubwa hapa nchini.

“Pia yupo Adebayor ambaye yeye huenda akajiunga na Berkane, hivyo sio tatizo kwetu hata kama tukiwakosa wachezaji wapo wachezaji wengine wengi Ukanda wa Afrika hivyo bado wachezaji wapo,” alisema Nghambi.

Imeandikwa na Dizo Click.

Previous articleSIMON MSUVA ATAJWA KUINGIA RADA ZA YANGA
Next articleUSAJILI UZINGATIE MAPENDEKEZO YA BENCHI LA UFUNDI