Home Sports GAMONDI APIGA MKWARA, YANGA HAO NUSU FAINALI

GAMONDI APIGA MKWARA, YANGA HAO NUSU FAINALI

MIGUEL Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga ameweka wazi kuwa licha ya kupata ushindi kwenye mchezo dhidi ya Tabora United bado hajafurahishwa na viwango vya wachezaji wake.

Kwenye mchezo huo uliochezwa Mei Mosi 2024 Yanga ilipata ushindi na kutinga hatua ya nusu fainali ndani ya CRDB Federation Cup ambapo wao ni mabingwa watetezi.

Tumecheza vizuri na kupata ushindi lakini bado sijafurahishwa na kiwango ambacho kimeonyeshwa hivyo tunaamini kwamba tutafanyia kazi makosa ili kuwa bora kwa mechi zinazofuata,”.

Ndani ya msimu wa 2023/24 Yanga inakwenda kukutana na Ihefu mara tatu katika mashindano mawili makubwa tofauti.

Ni mara mbili ndani ya Ligi Kuu Bara walipokomba dakika 180 kwa kila mmoja kutamba pande zake ndani ya uwanja.

Mchezo wa mzunguko wa kwamba ilikuwa Ihefu 2-1 Yanga na ule wa mzunguko wa pili Uwanja wa Azam Complex ilikuwa Yanga 5-0 Ihefu.

Ushindi wa Yanga 3-0 Tabora United katika robo fainali CRDB Federation Cup inawapelela Yanga hatua ya nusu fainali watamenyana na Ihefu katika msako wa timu itakayotinga fainali.

Mabao ya Yanga katika robo fainali Uwanja wa Azam Complex yalifungwa na Aziz KI, Kennedy Musonda na Joseph Guede.

Previous articleSIMBA MIKONONI MWA MTIBWA SUGAR
Next articleYANGA NA SIMBA MWENDO WA FAINI, ADHABU YA CHAMA NDOGO