Home Sports YANGA NA SIMBA MWENDO WA FAINI, ADHABU YA CHAMA NDOGO

YANGA NA SIMBA MWENDO WA FAINI, ADHABU YA CHAMA NDOGO

KAMATI ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu nchini imezitoza faini Simba na Yanga kutokana na kosa la kuingia katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kupitia milango isiyo rasmi siku ya mchezo wa KariakooDerby uliyochezwa April 20, 2024.

Kutokana na kosa hilo kamati imeitoza Yanga SC Shilingi milioni tano (5,000,000) baada ya kuonekana kutenda kosa hilo katika michezo zaidi ya minne (4) ndani ya misimu mitatu ya ligi kuu.

Klabu ya Simba pia imetozwa kiasi cha shilingi milioni moja (1,000,000) kutokana na kosa hilohilo walilolitenda siku ya mchezo wa NBC Premier League dhidi ya Yanga SC.

Katika taarifa hiyo pia mchezaji wa Simba SC, Clatous Chama amefungiwa michezo mitatu na kutozwa faini ya Shilingi milioni moja (1,000,000) kwa kosa la kumkanyaga kwa makusudi mchezaji wa Yanga, Nickson Kibabage katika mchezo huohuo.

Kutokana na adhabu hiyo ya Chama, Legend kwenye masuala ya michezo Bongo, Jembe amebainisha kuwa adhabu ya kiungo huyo ni ndogo hivyo ilipaswa kuongezwa zaidi kuwa somo kwa wengine.

Pia Jembe aliwashauri wachezaji kutambua namna ya kuwa walinzi kwenye mechi zote na kucheza fear kwa kuwa mchezo wa mpira sio vita.

Previous articleGAMONDI APIGA MKWARA, YANGA HAO NUSU FAINALI
Next articleAnza Alhamisi Yako na Meridianbet