Home Sports SIMBA MIKONONI MWA MTIBWA SUGAR

SIMBA MIKONONI MWA MTIBWA SUGAR

BAADA ya kugawana pointi mojamoja dhidi ya Namungo, Uwanja wa Majaliwa kete inayofuata kwa Simba ni dhidi ya Mtibwa Sugar.

Chini ya Kocha Mkuu Juma Mgunda akishirikiana na Seleman Matola mchezo wao wa kwanza kukaa benchi walishuhudia ubao ukisoma Namungo 2-2 Simba.

Timu hiyo ndani ya tatu bora haijawa na mwendo mzuri na itamkosa kiungo Clatous Chama ambaye amefungiwa mechi tatu kwa kosa la kumchezea faulo makusudi beki wa Yanga, Nickson Kibabage katika Kariakoo Dabi.

Ikumbukwe kwamba Mtibwa Sugar mchezo wake uliopita ilipoteza pointi tatu kwa kushuhudia ubao ukisoma JKT Tanzania 2-1 Mtibwa Sugar.

Ni Mei 3 2024 mchezo huo na unatarajiwa kuchezwa kwa kila timu kuoambania pointi tatu.

Previous articleANACHOMOLEWA KIUNGO WA KAZI YANGA
Next articleGAMONDI APIGA MKWARA, YANGA HAO NUSU FAINALI