
GABRIEL ANAWANYOOSHA TU
KIWANGO cha nyota wa Arsenal, Gabriel Jesus kimezidi kuwa moto baada ya wikiend kuweza kutupia mabao mengine. Ilikuwa ni kwenye mchezo dhidi ya Chelsea ambapo Arsenal iliweza kushinda kwa mabao 4-0 juzi huko jijini Orlando,Florida,Marekani. Raia huyo wa Brazil alifunga bao lake la nne ndani ya mechi nne za pre season na kuonyesha kwamba Arsenal…