Home Sports STARS KAMILI KUIVAA SOMALIA LEO

STARS KAMILI KUIVAA SOMALIA LEO

 KIM Poulsen Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania,Taifa Stars ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo kuwania kufuzu kuwania fainali za CHAN unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Ni Somalia watakuwa wenyeji kwenye mchezo wa leo na mchezo wa pili unatarajiwa kuchezwa Julai 30 ambapo Tanzania watakuwa wenyeji.

Mshindi wa jumla kwenye mchezo huu atacheza dhidi ya Uganda ili kupata mshindi atakayefuzu fainali za CHAN.

 “Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Somalia na tunaamini kwamba utakuwa ni mgumu ila tupo tayari kwa ajili ya kupata matokeo.

“Ni mchezaji mmoja ambaye hatakuwa kwenye mpango wetu David Luhende baada ya kupata maumivu ya misuli lakini wengine wapo vizuri,” amesema.

Previous articleRASTA WA MTIBWA SUGAR ATUA DODOMA JIJI
Next articleBEKI KMC KUIBUKIA RUVU SHOOTING