Home International GABRIEL ANAWANYOOSHA TU

GABRIEL ANAWANYOOSHA TU

 KIWANGO cha nyota wa Arsenal, Gabriel Jesus kimezidi kuwa moto baada ya wikiend kuweza kutupia mabao mengine.

Ilikuwa ni kwenye mchezo dhidi ya Chelsea ambapo Arsenal iliweza kushinda kwa mabao 4-0 juzi huko jijini Orlando,Florida,Marekani.

Raia huyo wa Brazil alifunga bao lake la nne ndani ya mechi nne za pre season na kuonyesha kwamba Arsenal imempata mfungaji waliyekuwa wanamhitaji.

Nahodha Martin Odegaard aliongeza bao kabla ya Bukayo Saka na Sambi Lokonga nao kuweza kufunga.

Kikosi cha Chelsea chini ya Thomas Tuchel kilionekana hakina ubora wa kutosha huku kikipungukiwa na hali ya kujiamini katika mchezo huo.

Beki wa kushoto Oleksandr Zinchennko aliyesajiliwa juzi kutoka Manchester City alicheza kwa kiwango kikubwa na kutimiza majukumu yake kwa wakati.

Previous articleIHEFU ITAKUWA NA CHIRWA,NYOSSO NA YONDAN
Next articleMANARA AFUNGUKIA ISHU YA KUFUNGIWA ATUMA OMBI KWA WAZIRI