Home Sports MANARA AFUNGUKIA ISHU YA KUFUNGIWA ATUMA OMBI KWA WAZIRI

MANARA AFUNGUKIA ISHU YA KUFUNGIWA ATUMA OMBI KWA WAZIRI

MSEMAJI wa Yanga Haji Manara ameongea na Waandishi wa Habari kuelezea sakata lake la kufungiwa kujihusisha na masuala ya michezo ndani na nje ya nchi kwa kipindi cha miaka 2 pamoja na faini ya shilingi milioni 20.

Manara amemtaka Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa kwenda kusimamia haki ya kiapo chake cha Katiba kwa kuhakikisha kanuni zilizotumika kumfungia zinakuwa ni kanuni halali ambazo zimesajiliwa

“Kwa minajili hiyo mimi na Mchengerwa wote Wandengereko na naamini wandengereko wote tunasimama na haki, Waziri wangu Mchengerwa kasimamie haki ya kiapo chako cha katiba kwamba huwezi kuruhusu haya.

Aidha Manara amesema yeye bado ni msemaji halali wa Yanga kwani hajapewa nakala ya hukumu yake ambayo ndiyo inampatia haki ya kukata rufaa.

Previous articleGABRIEL ANAWANYOOSHA TU
Next articleTFF YATOA TAMKO KUHUSU HAJI MANARA