
IHEFU ITAKUWA NA CHIRWA,NYOSSO NA YONDAN
BAADA ya mabosi wa Ihefu FC kumalizana na Obrey Chirwa inaelezwa kuwa anayefuata ni beki kitasa Kelvin Yondani ambaye ni mali ya Geita Gold. Ihefu ambayo msimu ujao itashiriki Ligi Kuu Bara inajiimarisha kwa ajili ya msimu mpya ikiwa ni mpango wa kufanya kweli ndani ya ligi kuepuka kushuka daraja kama ilivyokuwa msimu wa 2019/20…