
WANANCHI WAMEREJEA DAR, KUIBUKIA MWANZA
KIKOSI cha Yanga leo Novemba 11 kimerejea Dar na kinatarajia kuanza safari kuelekea Mwanza. Ni safari ya kutoka Tunisia ambayo ilianza jana Novemba 10 na walipitia Dubai kabla ya kuibukia Dar. Kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi kimetoka kupata ushindi wa bao 0-1 dhidi ya Club Africain na kutinga hatua ya makundi…