Home Sports WANANCHI WAMEREJEA DAR, KUIBUKIA MWANZA

WANANCHI WAMEREJEA DAR, KUIBUKIA MWANZA

KIKOSI cha Yanga leo Novemba 11 kimerejea Dar na kinatarajia kuanza safari kuelekea Mwanza.

Ni safari ya kutoka Tunisia ambayo ilianza jana Novemba 10 na walipitia Dubai kabla ya kuibukia Dar.

Kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi kimetoka kupata ushindi wa bao 0-1 dhidi ya Club Africain na kutinga hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika.

Miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa kwenye msafara huo ni pamoja na Kibwana Shomari, Aboutwalib Mshery, Farid Mussa.

Jumapili wana kazi ya kusaka pointi tatu kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Kagera Sugar unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa CCM Kirumba.

Ally Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema wamefurahi kurejea na ushindi ni zawadi kwa Watanzania.

“Tumerejea salama na ni furaha kwetu kuona tumepata ushindi ni zawadi kwa Watanzania na tuna kazi Mwanza Jumapili mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,” .

Previous articleMERIDIANBET YAWASHIKA MKONO HOSPITALI YA TUMBI
Next articleNUNUA TIKETI YA USHINDI KWENYE KASINO YA MTANDAONI YA MERIDIANBET