
YANGA: SASA NDIO MTATUELEWA, CHAMA ATOA TAMKO ZITO SIMBA SC
Yanga: Sasa ndio mtatuelewa, Chama atoa tamko zito Simba SC ndani ya Championi Ijumaa
Yanga: Sasa ndio mtatuelewa, Chama atoa tamko zito Simba SC ndani ya Championi Ijumaa
MAPEMA kabisa Desemba Mosi 2023 kikosi cha Simba kimekwea pia kueleka Botswana kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambao utakuwa ni wa pili kwao. Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 1-1 ASEC Mimosas hivyo waligawana pointi mojamoja na langoni alikaa Ayoub Lakred ambaye yupo…
TIMU ya Taifa ya Wanawake, Twiga Stars ipo kazini inapambania nembo ya taifa kwa kupata ushindi katika viunga vya Azam Complex kwenye mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya kuwania Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Wafcon) 2024. Ni dhidi ya Togo kwenye Uwanja wa Azam Complex, jijini Dar ambapo wameanza…
WAKALI wa pasi za mwisho ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2023/24 ikiwa ni mzunguko wa kwanza. Clatous Chama wa Simba msimu wa 2022/23 alikuwa kwenye ubora wake kwa sasa bado anajitafuta. Huku Clement Mzize akiwa miongoni mwa nyota wanaofanya vizuri ndani ya Yanga
Nahodha wa Manchester United, Bruno Fernandes, alikuwa na kiwango bora sana usiku wa mabingwa Ulaya kwenye mchezo uliomalizika kwa sare ya 3-3 dhidi ya Galatasaray ugenini. Man United walikwenda kwenye mchezo wakiwa na matumaini ya kupata pointi tatu na walianza vizuri wakiongoza 2-0 baada ya dakika 18 tu. Fernandes alitoa pasi ya ufunguzi kwa Rasmus…
UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa hesabu kubwa ni kupata ushindi kwenye mchezo wao ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AlAhly, Waarabu wa Misri. Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi inapeperusha bendera ya Tanzania katika Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa hatua ya makundi. Ikumbukwe kwamba ilitinga hatua hiyo kwa kuwafungashia virago Al…
NYAKATI ngumu hazidumu lakini zina maumivu makubwa kwa anayekutana nazo hivyo ni muhimu kutafuta njia nzuri ya kuepukana na hayo kwa umakini, hivyo tu basi. Wawakilishi wa Tanzania kwenye anga la kimataifa, Simba wanapita kwenye nyakati za maumivu kwa wachezaji kushindwa kupata ushindi katika mechi tatu za Ligi ya Mabingwa Afrika zaidi ya kuambulia sare….
TAARIFA kutoka ASEC Mimosas zimeeleza kuwa Yanga imefikia hatua nzuri ya mazungumzo kuhusu mchezaji Sankara Karamoko. Yeye ni mshambuliaji ambapo kama mambo yatakwenda sawa anaweza kuibukia ndani ya kikosi cha Yanga kuanza changamoto mpya.
KILA mmoja afanye kazi yake kwa wakati kutimiza majukumu yake. Katika anga la kimataifa wachezaji wengi wanatambua namna ushindani ulivyo. Hakuna ambaye anapenda kuona matokeo mabaya yanatokea uwanjani. Kwa sasa wachezaji wanakazi kufanya kweli kwenye mechi za kimataifa. Ni ushindani mkubwa kwa kila mechi kufanya kweli. Ukweli ni kwamba kushinda ndani ya uwanja kunahitaji mbinu…
KWA sasa kwenye vijiwe vya soka iwe mitandaoni mpaka mitaani ni kuhusiana na ujio wa kocha mpya wa Simba, Abdelhak Benchikha ambaye anatajwa kujiunga na Simba kwa dau kubwa. Taarifa za awali kupitia vyanzo visivyo rasmi vya Simba vimethibitisha kuwa kocha huyo ameigharimu Simba zaidi ya Shilingi Milioni 500 ili kumwaga wino kwenye timu hiyo…
Kombe la UEFA Europa League ni zito kuliko makombe yote ya UEFA yenye madini fedha licha ya kutokuwa na thamani kubwa sana, tofauti na vikombe vingine vinavyotolewa katika mashindano ya klabu barani Ulaya. Wiki hii kuna odds kubwa za mechi kubwa za Europa kama vile Atalanta vs Sporting Lisbon nk. Kombe hilo hukabidhiwa kwa timu…
KWA kitendo cha kukataa penalti wakamalia wakerwa na CR 7 wakiambulia makasiriko baada ya mkeka kuchanika kwenye mchezo huo ambao wengi waliamini timu ya mwamba huyo itashida. Cristiano Ronaldo, mshambuliaji wa Al Nassr FC juzi aliwashangaza watu kutokana na tukio lake la kukataa penalti. Timu yake ilipata penalti baada ya nyota huyo kufanyiwa faulo ndani…
MSHAMBULIAJI wa Singida Fountain Gate Meddie Kagere amesema kuwa ujumbe wake aliouandika kwenye fulana baada ya kufunga kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union ni aina ya ushangiliaji aliochagua. Novemba 27 Kagere alifunga bao lake la kwanza kwenye ligi na wakati wa kushangilia alionyesha fulana iliyoandikwa, “Mnafiki ishi naye kinafiki,”. Akizungumza mara baada ya mchezo huo…
KOCHA mpya wa Simba Benchikha amesema kuwa ni muhimu kufanya kazi kwa ushirikiano kufikia malengo ya timu hiyo huku akiweka wazi kuwa furaha yake kuwa katika timu hiyo ambayo ni kubwa Afrika. Kocha huyo ameweka wazi kuwa wanahitaji kufanya vizuri kufikia malengo ikiwa ni kutwaa ubingwa wa ligi ulio mikononi mwa Yanga.
NYOTA wa Yanga ikiwa ni pamoja na Maxi Nzengeli, Pacome Zouzoah, Zawadi Mauya, Kibwana Shomari wapo kamili kuwavaa Waarabu wa Al Ahly kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika. Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu Miguel Gamondi inashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na kete ya kwanza wakiwa ugenini walipoteza dhidi ya Waarabu wa Algeria. Kwa sasa…
WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa, Simba wameandika rekodi yao kwenye anga hilo kwa kukomba dakika 450 sawa na mechi tano bila kuambulia ushindi. Kwenye mechi hizo, mbili ilikuwa ni African Football League, (AFL) na tatu Ligi ya Mabingwa Afrika. Katika mechi tano, tatu wamecheza nyumbani na mbili ugenini. Katika mechi za AFL, ilikuwa…
MASHABIKI ni muhimu kufika uwanjani kwa ajili ya kushangilia mechi ambazo zinachezwa lakini ni muhimu kuwa makini na kuacha kufanya vurugu kwenye mechi husika. Afya ni muhimu kwa mashabiki ili kuendelea kusukuma gurudumu kwenye maisha ya kila siku. Ripoti za mashabiki kupigana ama kupigwa hazipendezi kuwa endelevu kwenye ulimwengu wa mpira. Ukweli ni kwamba kila…