Home Sports WAKATI WA KUWAJIBIKA NI SASA KWA KILA MMOJA

WAKATI WA KUWAJIBIKA NI SASA KWA KILA MMOJA

KILA mmoja afanye kazi yake kwa wakati kutimiza majukumu yake. Katika anga la kimataifa wachezaji wengi wanatambua namna ushindani ulivyo.

Hakuna ambaye anapenda kuona matokeo mabaya yanatokea uwanjani. Kwa sasa wachezaji wanakazi kufanya kweli kwenye mechi za kimataifa.

Ni ushindani mkubwa kwa kila mechi kufanya kweli. Ukweli ni kwamba kushinda ndani ya uwanja kunahitaji mbinu kubwa hasa katika mechi za kusaka pointi tatu.

Ili ushinde kimataifa ni lazima uwe makini kwenye kutumia nafasi ambazo zinatengenezwa kwa kuwa ni aghalabu sana kuzipata kwenye mechi kila baada ya dakika 90.

Ni dhahabu kubwa nafasi ambayo inatengenezwa kwa wachezaji lakini wanashindwa kuzitumia hili linapaswa kufanyiwa kazi kwa wakati ujao.

Kuwa kwenye mechi za kimataifa ni kazi kubwa inafanyika na kuwa ugenii ama nyumbani ni lazima kucheza kwa kujituma.

Zile kelele ambazo zinatokea nje ya uwanja ni kutokana na matokeo ambayo yanapatikana. Kikubwa zifanyiwe kazi kwa vitendo na wachezaji wenyewe.

Benchi la ufundi uzoefu pekee hautoshi kufanikisha malengo ya kutwaa mataji ama kupata pointi tatu zaidi ni kufanya kazi kwa ushirikiano kwenye kila hatua.

Ni muda mfupi ambao upo kukamilisha mechi za kimataifa hatua ya makundi lakini ni lazima kuwa na mpango kazi maalumu ambao utaleta matokeo mazuri.

Kila la kheri kwenye mechi zote ambazo zitachezwa kwa kupambana kufanya kweli muda ni sasa na inawezekana kufanya kweli.

Previous articleBENCHIKHA AKUMBUSHWE HAKUNA RAFIKI WA KUDUMU
Next articleANAKUJA YANGA MSHAMBULIAJI HUYU KUFANYA KAZI