Home Sports WAARABU WA YANGA WAPIGIWA HESABU KWA MKAPA

WAARABU WA YANGA WAPIGIWA HESABU KWA MKAPA

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa hesabu kubwa ni kupata ushindi kwenye mchezo wao ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AlAhly, Waarabu wa Misri.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi inapeperusha bendera ya Tanzania katika Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa hatua ya makundi.

Ikumbukwe kwamba ilitinga hatua hiyo kwa kuwafungashia virago Al Merrikh kwa ushindi wa jumla ya mabao 3-0.

 Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga, Ali Kamwe amesema kuwa wanatambua wana mechi ngumu lakini hesabu za nyumbani ni kupata ushindi.

“Ushindani ni mkubwa na kila timu inahitaji ushindi hilo lipo wazi. Katika mechi zetu tukianza na ule wa nyumbani dhidi ya Al Ahly mpango mkubwa ni kuona tunashinda.

“Al Ahly ambao ni mabingwa tunajua kwamba watakuja Uwanja wa Mkapa hao tutaanza nao kwa umakini na tahadhari kwani tunatambua ni timu yenye ubora kiasi gani lakini inakutana na timu ambayo ina malengo na kuhitaji matokeo,” alisema Kamwe.

Desemba 2 Yanga inatarajiwa kumenyana na Al Ahly Uwanja wa Mkapa ambapo na kete ya kwanza walipoteza kwa kufungwa mabao 3-0 dhidi ya CR Beluoizdad ya Algeria walio pamoja kundi D.

Previous articleSIMBA NA YANGA KIMATAIFA NI BALAA ZITO
Next articleBADO MANCHESTER UTD INA NAFASI YA KUFUZU 16 BORA