
TFF YAUFUNGULIA UWANJA WA CCM KIRUMBA, MWANZA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeufungulia uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza kutumika kwa michezo ya Ligi baada ya kufanya marekebisho yaliyokidhi vigezo vya kikanuni na sheria za mpira wa miguu. Taarifa ya TFF ya leo Machi 20, 2025 imeeleza kuwa Uwanja huo uliofungiwa kutokana na miundombinu yake kutofaa kutumika kama ilivyoainishwa kwenye masharti…