ARTETA YUPO ARSENAL MPAKA 2025

KLABU ya Arsenal imemuongezea dili jipya Kocha Mkuu Mikel Arteta hivyo atakuwa hapo mpaka mwaka 2025 akikinoa kikosi hicho kinachoshiriki Ligi Kuu England. Pia kocha wa timu ya Wanawake, Jonas Eidevall yeye atakuwa ndani ya timu hiyo mpaka msimu wa 2023/24 ndani ya timu hiyo. Arteta, alijiunga na timu hiyo mwaka 2019,ameweza kuiongoza timu hiyo…

Read More

MOURINHO WA AS ROMA AWEKA REKODI

JOSE Mourinho, Kocha Mkuu wa Klabu ya AS Roma ya nchini Italia Jose Mourinho ‘The Special One’ raia wa Ureno kaweka rekodi mpya kwenye ulimwengu wa michezo. Kocha huyo mbabe wa kauli ameweza kuzinoa timu mbali Ulaya ikiwa ni pamoja na FC Porto, Chelsea, Inter Milan, Real Madrid, Manchester United na Tottenham Hotspurs. Mourinho ameweka…

Read More

GUARDIOLA HANA UHAKIKA KABISA

KOCHA Mkuu wa Manchester City, Pep Guardiola amesema kuwa hana uhakika kuwa kama kipigo mbele ya Real Madrid kitaleta madhara ya kisaikolojia kwa wachezaji wake wa Manchester City kwenye mbio za kusaka ubingwa. City walitupwa nje na Real Madrid na baada ya kipyenga cha mwisho wachezaji walianguka uwanjani kwa huzuni baada ya kushuhudia faida ya…

Read More

JEZI YA MARADONA YAUZWA MKWANJA MREFU

JEZI ya nguli wa soka Duniani marehemu Diego Armando Maradona imeweka rekodi baada ya kuuzwa kwa kiasi cha Euro Milioni 7 kwenye mnada huko nchini Mexico ambayo ni sawa na kiasi cha Shilingi Bilioni 17,150,913,157 Jezi hiyo ndiyo iliyovaliwa na Maradona kwenye robo fainali ya Kombe la Dunia la mwaka 1986 iliyochezwa kwenye Uwanja wa…

Read More

FULHAM YAGAWA KIFURUSHI CHA WIKI

KLABU ya Fulham imetwaa ubingwa wa Ligi Daraja la Kwanza nchini Uingereza maarufu kama Championship. Fulham imechukua Ubingwa huo ikiwa katika Uwanja wake wa nyumbani Craven Cottage kwa kuichakaza Luton kwa jumla ya mabao 7-0. Fulham iliyoshuka daraja msimu uliopita kwa matokeo hayo sasa inapanda daraja na kurudi katika Ligi Kuu nchini Uingereza. Imecheza jumla…

Read More

REAL MADRID WATWAA TAJI LA 35

KLABU ya Real Madrid imetwaa taji la 35 la La Liga baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Espanyol wakiwa nyumbani. Taji hilo pia linamfanya Kocha Mkuu Ancelotti raia wa Italia kuwa kocha wa kwanza kutwaa mataji makubwa Ulaya katika ligi 5 bora. Aliweza kufanya hivyo England, Hispania, Ujerumani,Italia na Ufaransa. Nahodha Benzema alitupia…

Read More

SALAH ATWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA

MSHAMBULIAJI wa Klabu ya Liverpool raia wa Misri Mohamed Salah ametwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Ligi Kuu ya Uingereza kutoka kwa Shirikisho la Waaandishi wa Habari za Michezo nchini humo. Salah mwenye umri wa miaka 29 amekuwa na msimu mzuri akiwa na klabu yake ya Liverpool baada ya kufanikiwa kufumania nyavu mara…

Read More

MANCHESTER CITY WAPIGA 4G LEEDS UNITED

MANCHESTER City wakiwa na jambo lao hawazuilika baada ya wenyeji Leeds United kuchapwa mabao 4-0. Wakiwa Uwanja wa Elland Road mbele ya mashabiki 35,771 kichapo hicho hakikuepukika kwenye michezo wa Ligi Kuu England. Mabao ya Rodri dk 13,Nathan Ake dk ya 54, Gabriel Jesus dk 78 na Fernandinho dk ya 90+3 yalitosha kuwarejesha kileleni kwa…

Read More

WAKALA MAARUFU DUNIANI ATANGULIA MBELE ZA HAKI

WAKALA maarufu wa wachezaji raia wa Italia Mino Raiola amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda kwa miezi kadhaa. Wakala huyo aliyekuwa akiwasimamia wachezaji wakubwa duniani kama Paul Pogba na Zlatan Ibrahimovic amefariki akiwa na umri wa miaka 54. Raiola alilazwa katika hospitali ya Milan mnamo Januari 2022 na kufanyiwa upasuaji lakini aina ya ugonjwa…

Read More

LIVERPOOL KAZINI LEO DHIDI YA NEWCASTLE

KLABU ya Liverpool leo Aprili 30,2022 inatarajiwa kusaka pointi tatu mbele ya Newcastle United katika mchezo wa Ligi Kuu England. Ni katika Uwanja wa St James Park mchezo huo unatarajiwa kupigwa ambapo kila timu inahitaji ushindi. Liverpool ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 79 baada ya kucheza mechi 33 huku vinara wakiwa ni Manchester…

Read More

PSG WAGAWANA POINTI NA STRASBOURG

WAKIWA Uwanja wa de la Meinau wababe PSG waligawana pointi mojamoja na Strasbourg katika mchezo wa Ligue 1. Ilikuwa ni mabao ya Kevin Gameiro dk 3 Marco Verralti alijifunga dk 75 na bao la usiku lilifungwa na Anthony Caci dk 90+2. Kwa wababe PSG wao walifunga kupitia kwa Kylian Mbappe aliyetupia mabao mawili ilikuwa dk…

Read More

WAKALA RAIOLA ASEMA HAJAFA,YUPO

WAKALA mkubwa duniani Mino Raiola amelazimika kujibu mitandaoni akiwa kwenye kitanda kukanusha taarifa ambazo zimesambaa zikidai kwamba amefariki. Taarifa ziliibuka nyumbani kwao Italia ambapo zilieleza kuwa wakala huyo mkubwa amefariki baada ya kuugua. Ikumbukwe kwamba miongoni mwa wachezaji ambao anawasimamia ni pamoja na Paul Pogba,Erling Haaland ambao ni wachezaji wakubwa. Kumekuwa na meseji nyingi za…

Read More

MAJANGA SIMBA,KUSHTAKIWA CAF

MTENDAJI MKUU wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la nchini Afrika Kusini Tebogo Motlanthe amesema kitendo cha Klabu ya Simba kutoka Tanzania kuchoma kitu katikati ya Uwanja ni jambo la aibu na si la kiuanamichezo. Motlanthe amesema kitendo hicho hakikubaliki na tayari kama Shirikisho tayari wameandika barua kwenda Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF)…

Read More

MNYAMA RONALDO AFANYA YAKE

MBELE ya mashabiki 73,564 waliojitokeza Uwanja wa Old Trafford, Cristiano Ronaldo aliweza kufunga bao ambalo liliacha pointi moja kwa Manchester United. Ilikuwa dk ya 62 alisawazisha bao lililofungwa na Marcos Alonso wa Chelsea aliyefunga bao hilo dk ya 60. Hivyo wababe hao walikamilisha dakika 90 ubao ukisoma Manchester United 1-1 Chelsea. Ni Reece James wa…

Read More

KLOPP ANAAMINI NI MAPUMZIKO WAKIONGOZA 2-0

JURGEN Klopp,Kocha Mkuu wa Liverpool alikuwa shuhuda wa vijana wake wakiitungua mabao 2-0 Villarreal katika mchezo wa Nusu Fainali ya kwanza ya UEFA Champions League. Mbele ya mashabiki 51,586 katika Uwanja wa Anfield kipindi cha kwanza mambo yalikuwa ni magumu kwa timu zote mbili kwa kuwa halikupatikana bao. Ni Pervis Estupinan Tenorio alijifunga dk 53…

Read More