Home International MO SALAH KUUZWA LIVERPOOL

MO SALAH KUUZWA LIVERPOOL

IMERIPOTIWA  kuwa, Klabu ya Liverpool ipo tayari kumuachia, Mohamed Salah kama wakipata ofa nzuri kuanzia pauni 60m.

 Salah amesaliwa na mwaka mmoja katika mkataba wake ndani ya Liverpool, huku kwa muda mrefu wakivutana kwenye ishu ya mkataba mpya.

 Baada ya Sadio Mane kuondoka Liverpool hivi karibuni na kutua Bayern Munich, huenda pia wakampoteza na Salah.

 Imeelezwa kuwa, Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amekuwa akiangalia kwa ukaribu ishu ya nyota huyo inavyoendelea ndani ya Liverpool.

 Imeripotiwa kuwa, Salah anahitaji kulipwa pauni 400,000 kwa wiki kutoka pauni 240,000 anayolipwa kwa sasa ndani ya Liverpool.

 Msimu uliopita, Salah alifunga mabao 31 na asisti 16 katika michuano yote akicheza mechi 51.

 Salah alijiunga na Liverpool mwaka 2017 akitokea AS Roma, akiwa hapo ametwaa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Premier League, UEFA Super Cup, FA, Carabao na Klabu Bingwa Dunia.

Previous articleKIPA SIMBA AONGEZA MIAKA MIWILI
Next articleSTAA HUYU KUTOKA LEEDS UNITED MALI YA MAN CITY