Home Sports KIPA SIMBA AONGEZA MIAKA MIWILI

KIPA SIMBA AONGEZA MIAKA MIWILI

KIPA namba moja wa kikosi cha Simba ambacho kwa sasa kipo chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Seleman Matola Aishi Manula ameongezewa mkataba wake wa kuendelea kuitumikia timu hiyo.

Nyota huyo mkataba wake ulikuwa unakaribia kufikia ukingoni na kuna timu ambazo zilikuwa zimeanza mazungumzo naye kwa ajili ya kuinsa saini yake.

Manula ambaye ni chaguo la kwanza ndani ya kikosi cha Simba kwa sasa hajacheza kwenye mechi za ligi kutokana na kuwa na matatizo ya kifamilia na nafasi yake ipo mikononi mwa kipa namba mbili, eno Kakolanya.

Taarifa zimeeleza kuwa Manula ameongeza mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu hiyo ambayo kwa sasa inafanya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa kesho Juni 29 wa ligi dhidi ya Mbeya Kwanza.

Manula msimu huu amecheza mechi 21 kafungwa mabao 11 na hajafungwa kwenye mechi 11baada ya kutumia dk 1,890.

Previous articleMWAMBA HUYU HAPA ANATUA YANGA,NDANI YA SPOTI XTRA JUMANNE
Next articleMO SALAH KUUZWA LIVERPOOL