Home International TUCHEL ANAMTAKA LEWANDOWSKI

TUCHEL ANAMTAKA LEWANDOWSKI

KOCHA Mkuu wa klabu ya Chelsea raia wa Ujerumani Thomas Tuchel ameisisitizia Bodi ya klabu hiyo kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha inapata saini ya mshambuliaji hatari wa Bayern Munich na Timu ya Taifa ya Poland Robert Lewandowski.

Tuchel anatamani Lewandowski achukue mikoba ya Romelu Lukaku ambaye anatazamiwa kujiunga na klabu yake ya zamani ya Inter Milan kwa mkopo mapema wiki ijayo hii ni kutokana na kuwepo kwa maendeleo mzauri katika mazungumzo yanayomhusisha mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United.

Thomas Tuchel amekuwa akivutiwa na Lewandowski kwa muda mrefu, mchezaji huyo ameshaweka bayana adhima yake ya kuondoka kwenye viunga vya Allianz Arena na anaamini anaweza kufanya vizuri katika ligi kuu ya Uingereza licha ya kutimiza umri wa miaka 34 mwezi Agosti mwaka huu.

Endapo Lewandowski akifanikiwa kusaini na klabu ya Barcelona basi Chelsea itahamishia macho yake kwa mshambuliaji mwingine ingawa hadi sasa haijulikani macho yataelekea kwa mchezaji gani.

Kulikuwa na taarifa za Chelsea kuhusishwa na usajili wa mshambuliaji wa Manchester City Gabriel Jesus lakini kwa mujibu wa taarifa zilizopothibitishwa na Skysports ni kwamba klabu ya Arsenal ipo katika hatua nzuri ya kumalizana  na mshambuliaji huyo raia wa Brazil kwa kitita cha Paundi milioni 55.

Previous articleVIDEO:MSHAMBULIAJI HUYU TP MAZEMBE AINGIA ANGA ZA SIMBA
Next articleMCHEZO MZIMA WA AZIZ KI KUSAINI YANGA UPO HIVI