Home Sports MCHEZO MZIMA WA AZIZ KI KUSAINI YANGA UPO HIVI

MCHEZO MZIMA WA AZIZ KI KUSAINI YANGA UPO HIVI

SAKATA la usajili wa kiungo mshambuliaji wa ASEC Mimosas ya Ivory Coast, Stephanie Aziz Ki, limeingia katika sura mpya na kumuibua Msemaji wa Yanga, Haji Manara ambaye amefunguka kila kitu kuhusu ishu ya staa huyo kutua Jangwani.

Aziz Ki amekuwa gumzo kubwa kwa siku za karibuni kufuatia kuziingiza kwenye vita kali klabu za Simba na Yanga ambazo zote zimeonesha nia ya kuhitaji saini yake, ambapo inaelezwa kuwa tayari Yanga wamemalizana naye.

Staa huyo alijiunga na ASEC Mimosas Januari 2021, ambapo kwenye michuano ya kimataifa pekee msimu huu wa 2021/22 ameifungia timu hiyo mabao manne akicheza michezo 10.

Akizungumzia usajili wa staa huyo ndani ya Yanga, Manara alisema: “Unajua watu wengi wanakosea, sisi hatujaanza kumfuatilia Aziz Ki mara baada ya kucheza dhidi ya Simba, tumeanza kumfuatilia tangu Agosti mwaka jana ila kilichokwamisha ni kwamba tayari alikuwa amesaini mkataba na ASEC,” .

Previous articleTUCHEL ANAMTAKA LEWANDOWSKI
Next articleSIMBA KAMILI KUIVAA KMC