Asia Mustapha Afariki Baada ya Kuishi Miaka 20 Bila Figo
Habari mbaya zilizotufikia asubuhi hii ya Desemba 24, 2025 zinaeleza kuwa, mwanadada Asia Mustapha aliyesumbuliwa na figo kwa zaidi ya miaka 20 amefariki dunia. Taarifa zilizothibitishwa na ndugu zake zinaeleza kuwa, Asia amekutwa na umauti usiku wa kuamkia leo alipokuwa amelazwa wodi ya wagonjwa mahututi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam….