Yanga SC yakwea pipa baada ya kumalizana na Simba SC
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa na NBC, Yanga SC chini ya Kocha Mkuu Romain Folz wamekwea pipa kuelekea Angola kwa mechi ya kimataifa Ligi ya Mabingwa Afrika. Septemba 16 2025 saa 11:00 jioni, Yanga SC walikuwa na kazi kutetea taji la Ngao ya Jamii katika mchezo wa fainali dhidi ya Simba SC…