Simba SC hesabu zimehamia CRDB Cup

BAADA ya kufunga msimu wa 2025/26 wakiwa nafasi ya pili na pointi 73, uongozi wa Simba SC umebainisha kuwa mpango mkubwa kwa sasa ni mechi ya fainali dhidi ya Azam FC.

Simba SC ilifunga msimu wa 2025/26 kwa kupata ushindi wa bao 1-0 KMC FC uliochezwa Juni 30,2026 Uwanja wa KMC Complex.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema msimu umeisha kwenye ligi wakikwama kufikia malengo ya kutwaa ubingwa hivyo hesabu kubwa ni mchezo wa fainali.

Matumaini ya Simba SC kutwaa taji kwa msimu wa 2025/26 yamebaki kwenye CRDB Federation Cup ambalo hata Azam FC wanalihitaji pia.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Julai 4,2026 kwa wababe hawa kusaka taji ukiwa ni mchezo wa funga msimu jumlajumla.

“Tumemaliza msimu tayari na tumekosa ubingwa wa ligi hilo tunasahau na sasa nguvu kubwa ni kuelekea mchezo wetu wa fainali ya CRDB Federation Cup.

“Mashabiki wazidi kuwa nasi katika kila hatua malengo ni kuona tunapata ushindi kwenye mchezo wetu mgumu na tupo tayari,”.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.