NYOTA WATANO SIMBA WATAPIGWA PANGA
SIMBA huenda ikaachana na wachezaji watano mwishoni mwa msimu huu mara baada ya mikataba yao kumalizika,kati ya hao yupo beki Muivory Coast, Pascal Serge Wawa. Hiyo ni katika kuhakikisha wanakuwa na kikosi imara kitakachofanya vizuri msimu ujao kwenye mashindano mbalimbali. Tayari uongozi wa Simba umeanza kufanya mazungumzo na baadhi ya wachezaji wapyawatakaowasajili.Mmoja wa mabosi wa Simba, ameliambia Spoti Xtra kuwa, wachezaji hao baadhi wataachwa kutokana na umri mkubwa walionao….