LIGI ya Beach Soccer imeendelea leo katika viwanja vya Coco Beach ambapo mechi za makundi mawili A na B zilichezwa.
Ulianza mchezo wa Kundi A kati ya Ilala v PCM ambapo baada ya mchezo kukamilika ubao ulisoma Ilala 7-7 PCM na mshindi alipatikana kwa penalti na ni Ilala ilishinda penalti 5-3 PCM.
Mchezo wa kundi B ulianza ule wa Sayari dhidi Mburahati na Sayari ilipata mabao 3-4 Mburahati.
Katika mchezo wa pili wa kundi B katika Ligi ya Beach Soccer inayodhamiwani na Global Online uliwakutanisha Kijitonyama v Mshikamano FC na ulikamilika kwa Kijitonyama kushinda mabao 9-3.
Mchezo wa mwisho ulikuwa kati ya Kisa FC 2-4 Friends Ragers ambapo kwa timu ambazo zimeshinda zimetoa zawadi ya Pasaka kwa mashabiki wao.