Home International U 17 WAMEANZA MWENDO,WAUNGWE MKONO

U 17 WAMEANZA MWENDO,WAUNGWE MKONO

HATUA moja kila wakati tunaona kwa timu ya Taifa ya Wanawake chini ya Miaka 17 kwa namna ambavyo wanafanya vizuri kwenye mechi za kuwania Kufuzu Tiketi ya Kombe la Dunia.

Pongezi kwa Serengeti Girls baada ya kuweza kupata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Burundi mchezo uliochezwa Uwanja wa Urukundo,Ngozi nchini Burundi.

Haukuwa mchezo mwepesi hasa kutokana na wenyeji nao kuwekeza nguvu kubwa kwenye kusaka ushindi kwa kuwa kila timu inahitaji kuweza kupata nafasi ya kushiriki Kome la Dunia.

Tanzania tuna vipaji vilivyo na kila mchezaji kujitoa kwa ajili ya Tanzania kuhakikisha kwamba inaweza kupata kile ambacho inastahili ambacho ni matokeo na wanapambana kweli katika hilo.

Ninapenda kuwapa pongezi na kuwaambia kwamba kazi bado inaanza kwa kuwa hapa ambapo wapo wanapaswa kuendelea kupata matokeo bilakuchoka kwa kuwa ushindani ni mkubwa.

Kwa mechi za ugenin kupata ushindi mkubwa hilo ni jambo ambalo linapaswa kupongezwa kwa wachezaji pamoja na benchi la ufundi kwa namna ambavyo wanawapa mafunzo vijana wao.

Ukweli ni kwamba makossa ambayo yanafanyika hasa ya kukosa nafasi ambazo zinatengenezwa nina amini kwamba yatafanyiwa kazi kwenye mechi zijazo.

Hatua hii ni kubwa na hatua ijayo nayo ina umuhimu kwa kuwa ili timu iweze kusonga mbele lazima ipate matokeo chanya kwenye mechi zake zote.

Hapa Burundi ninaona kwamba watakuwa wamepata funzo kwa namna ambavyo Serikali imeweza kuwa bega kwa began a Shirikisho la Soka Tanzania.

Tangu mwanzo wa mazoezi mpaka mwisho bado hatua ubwa zilikuwaz zinaoneana kwa Serikali kuwa bega kwa began a wachezaji pamoja na viongozi.

Hili ni jambo kubwa kwa kuwa kupata matokeo ni jamo lingine na sapoti pia kutoka kwa wahusika wenyewe hasa Wizara ya Michezo inaongeza nguvu kwa vijana kwa wakati ujao kuweza kufanya vizuri zaidi.

U 17 hawa ni kizazi kipya ambacho kina muda wa kufanya vizuri kwa wakati ujao hivyo muda huu kinajengwa upya na kwa umakini mkubwa.

Hakuna ambaye amekuwa akionyesha nia ya kukata tamaa bali morali imekuwa kubwa kwa kila mmoja hasa kuanzia kwenye mazoezi na kwenye mechi za ushindani.

Watanzania tuzidi kuiombea dua timu hii ili iweze kufanya vizuri kitaifa na kimataia kwa kuwa mafanikio ya U 17 Ni faida kwa Tanzania.

Ikiwa itafanikiwa kukata tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia  ambalo linatarajiwa kuweza kuchezwa kuanzia Oktoba 11 nchini India ni fursa kwa wachezaji wetu kuweza kupata ajira.

Watafungua njia ya kuongeza nyota wengine ambao watakuwa wanacheza soka la kulipwa na hili litaongeza thamani ya mpira wetu.

Kwa hapa bado jitihada zainahitajika kwa kuwa ushindani ni mkubwa na kila timu inahitaji kupata ushindi kwenye mechi yake.

Previous articleKAGERA SUGAR YAGAWANA POINTI NA KMC,KAITABA
Next articleKOCHA ORLANDO PIRATES AGOMEA USHINDI WA SIMBA