KIMATAIFA MAMBO BADO UWANJA WA MKAPA

MAMBO ni magumu Uwanja wa Mkapa dk 45 za kipindi cha kwanza mchezo wa Kombe la Shirikisho.

Simba 0-0 Orlando Pirates na asilimia ni 59 kwa umiliki wa mpira mwa Simba na Pirates ni asilimia 41.

Ni kona 4 Simba wamepiga huku Orlando Pirates wao wakipiga kona moja ndani ya dk 45 za kipindi cha kwanza.

Hakuna aliyeweza kuotea kwa timu zote mbili leo ndani ya dk 45 huku Simba wakionekana kukosa utulivu eneo la mbele katika kumalizia nafasi ambazo wanazipata.

Ni Bernard Morrison ambaye ameonekana kuwa mwiba kwa Orlando Pirates licha ya kushindwa kuipa matokeo timu yake Uwanja wa Mkapa.