TEN HAG AAMBIWA ALIKOSEA KUPANGA KIKOSI

CHAMBUZI wa masuala ya michezo Jamie Redknapp amemlaumu Kocha Mkuu wa Manchester United,Eric ten Hag kwa kipigo cha mabao 4-0 dhidi ya Brentford ugenini kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa Jumamosi.

United walipata tabu kwenye mchezo huo kwa mabao ya Josh Dasilva,Ben Mee,Bryan Mbuemo na Mathias Jensen.

Licha ya kwamba kuna makosa ya washambuliaji wa United pamoja na makosa ya mchezaji mmojammoja yaliyosababisha mabao hayo Redknapp anasisitiza kwamba Ten Hag ndiye aliyefanya makosa kwenye Uwanja wa Gtech Community.

“Brentford walikuwa bora sana kwa United. Kuna mtu anatakiwa kuwajibika sikuamini ambacho nilikuwa ninakiona kocha alifanya makosa.

“Eriksen hawezi kucheza kama kiungo mkabaji na Martinez hana uimara wa kutosha na hataweza kushindana katika ligi hii ya England anaweza kuwa sawa kwenye ligi ya Uholanzi,” aliiambia Sky Sport.