TWIGA STARS YAKIRI KUFANYA MAKOSA,KESHO KUFANYA KWELI

KOCHA wa Timu ya Taifa ya Wanawake, Twiga Stars, Bakari Shime, amesema walifanya makosa
kwenye mchezo uliopita
wakiwa nyumbani na sasa wanakwenda kuwafunga Namibia wakiwa kwao, kesho Jumamosi.


Twiga Stars walichapwa 2-1
na Namibia kwenye mchezo wa kusaka tiketi ya kwenda Afcon
mwakani, kwenye mtanange
uliochezwa Jumatano Uwanja wa Mkapa, Dar.


Akizungumza na
Championi Ijumaa, Shime alisema walifanya makosa kwenye mchezo uliopita, wameliona hilo na watakwenda kulifanyia kazi wakiwa ugenini ambako kwa namna yoyote lazima wapate ushindi.

Tayari kikosi cha Twiga Stars kipo nchini Namibia na kimefanya maandalizi ya mwisho kwa ajili ya mchezo huo unaoatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.