HAZARD AWEKWA RADA ZA CHELSEA

NYOTA wa Real Madrid, Eden Hazard ambaye mambo kwake yamekuwa magumu ndani ya kikosi hicho anatajwa kuingia kwenye rada za Newcastle pamoja na Chelsea.

Nyota huyo hana furaha ndani ya Real Madrid kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara jambo ambalo limefanya ashindwe kuwa kwenye ubora ambao alikuwa nao alipokuwa akicheza ndani ya kikosi cha Chelsea.

Kocha wa Madrid, Carlo Ancelotti amekiri kuwa hana hesabu za kuendelea kumtumia nyota huyo hivyo anaongeza nafasi kubwa kwa Hazard kuweza kusepa katika kikosi hicho kinachoshiriki La Liga.

Ancelotti aligonga msumari mwingine wa nguvu kwa kusema kwamba ni bora asajili mchezaji mwingine kuliko kumtumia Hazard ambaye usajili wake uligharimu pauni milioni 89 na ripoti zinaeleza kuwa Chelsea ipo tayari kutoa pauni milioni 42 kumpata mchezaji huyo mwenye miaka 30.