KITAWAKA LEO SPURS V UNITED,POGBA ‘OUT’

LEO Oktoba 30 kutakuwa na mchezo mkali wa Ligi Kuu England ambapo Manchester United watakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Tottenham Hotspur.

 

Manchester United wamekuwa kwenye mwendo wa kusuasua hivi karibuni sawa na Spurs pia nao hawapo vizuri licha ya kupewa nafasi ya kusinda mchezo wa leo utakaopigwa saa moja usiku.

United yenye Cristinao Ronaldo kumbukumbu zao kwenye mchezo wao uliopita walinyooshwa mabao 5-0 mbele ya Liverpool wakiwa kwenye chimbo lao pale Old Trafford jambo ambalo linaamanisha kwamba mchezo wa leo ni ngoma ngumu kwa Kocha Mkuu wa United, Ole Gunnar Solkjaer ambaye anaweza kutimuliwa ikiwa atachapwa tena.

Spurs ambao nyota wao ni  pamoja na Harry Kane wao wamepoteza michezo minne waliyocheza kati ya sita ndani ya Ligi Kuu England huku United ikipoteza mitatu hivyo nyasi zitawaka leo Uwanja wa Tottenham.

Habari njema kwa mashabiki wa Manchester United ni kwamba nyota wao Raphael Varane yupo fiti kwa sasa hivyo anaweza kukiwasha beki huyo ila watakosa huduma ya Paul Pogba ambaye alionyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo uliopita dhidi ya Liverpool.

Wenyeji Spurs wao Bryan Gil wanaweza kuwa naye ila Ryan Sessegnon hatakuwa kwenye sehemu ya kikosi.