Real Betis watawapokea Real Madrid ya Kocha Jose Mourinho katika uwanja wao wa Estadio de La Cartuja jijini Seville, usiku wa leo Ijumaa Septemba 4, 2026, huu ni mchezo wa mzunguko wa nne wa La Liga Uhispania.
Real Betis wameanza msimu vizuri, wakishinda mechi mbili kati ya tatu za mwanzo walishinda dhidi ya Real Sociedad na Valencia kwa magoli 1-0 kila mmoja. Hata hivyo, kasi yao ilizimika wikendi iliyopita walipofungwa vibaya mabao 5-2 na Levante, hali inayoonyesha udhaifu wa ulinzi wao. Timu hiyo kwa sasa inashika nafasi ya saba katika msimamo, ikiwa na pointi sita.
Real Madrid kwa upande wao wameonyesha nguvu kubwa chini ya uongozi mpya wa kocha Jose Mourinho, wakishinda mechi zote tatu za mwanzo dhidi ya Espanyol (2-1), Real Sociedad (4-1), na Malaga (4-0).
Real madrid wakithibitisha ubora wao wa kujenga mashambulizi mapema msimu huu, na wanaendelea kuwania nafasi ya juu sambamba na wapinzani wao wakubwa Barcelona.
Kihistoria, Real Madrid wana ubora mkubwa dhidi ya Betis. Katika mechi nne za hivi karibuni kati yao, Betis wameshinda mara moja tu nyumbani. Mchezo wa mwisho Bernabéu uliishia kwa ushindi mkubwa wa Madrid wa mabao 5-1.
Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema. Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Wakati mechi ya mwisho Seville iliishia sare 1-1, ikionyesha kuwa Betis wanaweza kuwa wagumu kuwafunga wanapocheza nyumbani hata dhidi ya wapinzani wakubwa.
Timu ya Betis itaingia uwanjani ikiwa na changamoto za majeruhi wakiwemo Isco na Nabil Fekir, jambo linaloweza kuathiri ubunifu wao mbele.
Hata hivyo Real Madrid wanajipanga vizuri kabla ya mechi yao ijayo ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Inter Milan wiki ijayo, lakini wanatarajiwa kuwa makini kuepuka kupoteza pointi dhidi ya timu iliyomaliza nafasi ya tano msimu uliopita na kufuzu Ligi ya Mabingwa.